TTCL

EQUITY

Saturday, December 6, 2014

SFW 2014 yaanza kwa kishindo jijini Dar es Salaam

Maonesho makubwa ya mavazi, Swahili Fashion Week yamefanyika kwa mafanikio makubwa katika siku yake ya kwanza katika Hoteli ya Sea Clif Jijini Dar es Salaam na kuhudhiriwa na umati wa wadau mbalimbali katika sekta ya mitindo na burudani.

Collection ya Mitindo kutoka Africa Dandrl jukwaani
Katika onesho hili ambalo lilishereheshwa na mtangazaji na mtayarishaji vipindi mahiri kutoka EATV, Bi Bhoke Egina, wabunifu Ailinda Sawe, Afrikadndrl, H&A Dress to Impress, Mabinti Centre, EDC, Handmade TZ and Can Wear na Sabina Mutsvasi walionyesha collection ya mitindo yao.
Hii inakuwa ni siku ya kwanza kwa maonesho haya makubwa ambayo yatafanyika pia siku ya leo na Jumapili ambapo sambamba na maonesho kutakuwa na tukio kubwa la ugawaji tuzo kwa wadau mbalimbali waliofanya vizuri katika vipengele mbalimbali kwa upande wa mitindo.

No comments:

Post a Comment