TTCL

EQUITY

Wednesday, November 5, 2014

Meya anayetuhumiwa kuua akamatwa Mexico

Meya Jose Luis Abarca na mkewe Maria de los Angeles Pineda wamekuwa wakitafutwa wakihusishwa na kupotea kwa wanafunzi
Polisi nchini Mexico wamemkamata meya wa mji wa Iguala, pamoja na mke wake ambako wanafunzi 43 walipotea mwezi Septemba.
Jose Luis Abarca ambaye amekuwa akitafutwa amekamatwa na maafisa wa polisi katika mji mkuu wa Mexico, Mexico City.
Maafisa wa Mexico wamemtuhumu Bwana Abarca kwa kuwaamrisha polisi kupambana na wanafunzi katika siku ya kutoweka kwao tarehe 26 Septemba.
Watu walioshuhudia tukio hilo wameeleza kuwaona wanafunzi wakipakiwa katika magari ya polisi.
Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto amepongeza kazi nzuri ya waendesha mashtaka na majeshi ya usalama.
Majirani washangaa kuona kuwa Bwana Abarca na mkewe walikuwa wakiishi katika nyumba hiyo.
"Natumaini kukamatwa kwao kutafumbua mambo mengi ambayo yanachunguzwa na waendesha mashitaka wa serikali" amesema Bwana Pena Nieto.
Maafisa wa Mexico walitoa amri ya kukamatwa kwa Bwana Abarca na mkewe, Maria de los Angeles Pineda, baada ya maafisa wa polisi wa mji wa Iguala kusema walipewa amri kutoka kwa meya wa mji huo kupambana na wanafunzi.
Maafisa hao wanasema waliambiwa kuwazuia wanafunzi wasivuruge hotuba ya Bi Pineda katika mji wa Iguala siku hiyo.
"Huu ndio upande uliokuwa ukikosekana. Kukamatwa kwao kutasaidia kuwapata watoto wetu," Felipe de la Cruz, mzazi wa mmoja wa watoto waliopotea ameiambia televisheni ya Milenio.
Picha za wanafunzi waliopotea Iguala, Mexico
Majirani wamesema hawakuwa na fununu kuwa Bwana Abarca na mkewe walikuwa wakiishi katika nyumba hiyo.
Kupotea kwa wanafunzi 43 kumechochea maandamano makubwa.
Wanafunzi hao kutoka chuo jirani cha mafunzo ya Ualimu, walisafiri kwenda Iguala kuchangisha na kuandamana.
Tangu siku hiyo hawajaonekana. Harakati za kuwatafuta wanafunzi hao kulifichua uwepo wa makaburi ya pamoja katika eneo hilo, lakini majaribio ya kwanza yalionyesha kuwa si ya wanafunzi.
Tangu wakati huo, miili zaidi imegunduliwa na maafisa wametilia mashaka kuhusu uhakika wa majaribio hayo.
Uchunguzi zaidi wa miili hiyo unafanyika.

No comments:

Post a Comment