TTCL

EQUITY

Monday, November 24, 2014

MATUKIO YA WIZI WA WATOTO YAONGEZEKA KILIMANJARO

Matukio ya wizi wa watoto Mkoani Kilimanjaro yameongezeka kutoka watoto wanne mwaka 2013 hadi watoto 127 mwaka huu,hali ambayo imezua hofu kwa wazazi na wakazi na Mkoa huo.

Mratibi wa kupingana na ukatili wa kijinsia kanda ya Kaskazini Hilary Tesha alisema takwimu hizo ni kuanzia January hadi November mwaka huu

Tesha alisema wizi wa watoto umekua ukihusishwa na imani za kishirikina na sasa unaonekana kuanza kuota mizizi.

Alisema imefika wakati kwa jamii kutoa taarifa mara wanapoona ama kugundua mtandao unaohusika na utekaji watoto na mbali na hilo pia matukio ya ubakaji yameongezeka kutoka matukio 24 hadi 31 kwa mwaka.

Alisema chanzo cha matukio hayo yanasababishnwa na matumizi ya dawa za kulevya ndani ya jamii zinazotuzunguka na kuongezaka unywaji pombe kiholela.

No comments:

Post a Comment