TTCL

EQUITY

Tuesday, November 25, 2014

Binadamu kabla hujafa hujaumbika....




Kama ulishawahi kuchukia na namna mwili wako ulivyoumba tofauti na wengine, basi Claudio Vieira de Oliveira atakupa hisia tofauti za kimtizamo.
Ana miguu isiyo ya kawaida, hawezi kutumia mikono na viganja vyake, na kichwa chake kiko juu – chini.

Claudio, 37, alizaliwa akiwa na matatizo, akiwa na umbo la ajabu kiasi ambacho mama yake alishauriwa na madaktari amuache afe. Kwa bahati, hakuwasikiliza, na kijana wake amekwenda na kuithibitishia dunia kwamba anaweza kufanya chochote ambacho mtu yeyote anaweza kufanya, na huenda akafanya vizuri zaidi.

Mama yake alisema: “Watu walianza kusema “mtoto atakufa” kwa sababu hakuweza kupumua vizuri wakati alipozaliwa. Baadhi ya watu walisema ‘usimlishe”, ameshakufa tayari.

Claudio Vieira de Oliveira anayeishi Brazil anasema haoni tofauti aliyokuwa nayo na binadamu wengine.

Claudio Vieira de Oliveira anayeishi Brazil anasema haoni tofauti aliyokuwa nayo na binadamu wengine.

Ila kwa sasa, akiwa amejifundisha namna ya kujitegemea kwa kiasi kikubwa, na anajichukulia kama binadamu wa kawaida. Ni mzungumzaji wa hamasa na pia ana shahada (digrii) katika uhasibu.

Claudio, ambaye anaishi Brazil, alisema: “Tangu nilipokuwa mdogo nilipenda kujibidiisha na kufanya kazi – sipendi kuwategemea watu kabisa.

“Nimejifunza kuwasha televisheni, kutumia simu yangu, kuwasha redio, kutumia mtandao, kompyuta yangu- yote nayafanya mimi mwenyewe.”


Aliongeza: “Katika maisha yangu nimeweza kuuzoesha mwili wangu na ulimwengu. Kwa sasa, sijichukulii kama mtu tofauti. Mimi ni mtu wa kawaida.”



No comments:

Post a Comment