TTCL

EQUITY

Tuesday, May 20, 2014

MASTAA WAKUBWA WAKIKE WA BONGO MOVIE WALIOJARIBU UBUNGE 2015

Msanii wa Filamu za kibongo, Wema Abraham Sepetu, aliyekuwa anagombea Ubunge wa Viti Maalum jimbo la Singida amebwagwa chini baada ya kupata kura 90 tu katika uchaguzi huo.


 

binti ya mpiga picha na blogger maarufu nchini anayeambatana na rais Kikwetekatika ziara zake, Muhidin Issa Michuzi Bi. Zahara Michuzi alishindwa kupata kura za kutosha kumwezesha kushinda nafasi ya ubunge wa vijana kupitia tiketi ya CCM mkoa wa Tabora baada ya msanii wa filamu Bi. Irene Uwoya kupata kura 34 kati ya 39 zilizopigwa.

aidha wajumbe walimshangilia sana na kumpongeza kwa ukomavu wa kisiasa aliouonesha ambapo mwenzie Mariam Shamte alisusia na kuondoka ukumbini. mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Bw. Hassan Wakasuvi aliwaeleza wajumbe kuwa Obama alizaliwa na baba raia wa Kenya na mama Mmarekani lakini leo hii anaiongoza Marekani, hivyo wasione ajabu kama pana mgombea asiyetokea Tabora kiasilia. Bila shaka alikuwa akimzungumzia Irene Uwoya ambaye kabla ya uchaguzi wakazi wengi wa Tabora walielekea kutomkubali kwa kusema kwa nini CCM ituletee mgombea tokaArusha, Moshi au Dar es Salaam, na kwanini Irene asigombee Dar au Arusha? waliendelea kuhoji kuwa ni vipi Irene atayajua matatizo ya vijana wa Tabora ambao hawajui wala hana uelewa na mkoa huo? Lakini hayawi hayawi hatimaye yamekuwa kwa Irene ameibuka mshindi katika kinyang'anyiro hicho. Kama maneno ya Mwenyekiti huyo wa CCM mkoa wa Tabora yalifanya kazi kusababisha Irene Uwoya achaguliwe kwa kishind, lakini gafla ikadaiwa jina lake liliondolewa baada ya kupelekwa makao makuu dodoma.

No comments:

Post a Comment