TTCL

EQUITY

Friday, January 3, 2014

Haya ndio yanayo tendeka kwenye Ofisi zetu

Mini-skirts have become a norm on dress down Friday as many people gear up for the night ahead and hit the town straight after work


Kumekuwa na kero mbalimbali pindi tunapoenda kwenye ofisi mbalimbali kupata huduma katika ofisi hizo na hizi ndizo sababu zinazofanya wafanya kazi wangi wasiwe makini na kazi walizopewa na waajiri wao.
 
     Ø  Mapenzi kazini;
Kiza hiki cha digital mapenzi yamekuwa wazi wazi na sio kificho tena kama wazee wetu wazani walikuwa wanafanya mambo yao kwa siri sana lakini hivi sasa vijana hawajali wapo wapi hata maofisini sasa wanatumia kufanya uchafu wao haijalishi ni mfanyakazi mwenzake au kutoka nje ya ofisi. Imefikia hatua wafanyakazi wanafanya mapenzi hata kwenye vyoo ya ofisi. Maofisini sasa kumekuwa hakuna amani tena maana haijaalishi ni mke/mume wa mtu wote wamekuwa ni wafuska tu.
 
Huko ndiko baadhi ya ndoa zimevunjika kutokana na kusalitiana wakiwa kazini. Ndio maana wanaume wangine wanawaachisha kazi wake zao baada ya kuona mienendo ya wake zao kuwa mibaya. Na baadhi ya maboss wa siku hizi wamekuwa na tamaa sana kutembea na wafanyakazi wake kwa kuwa ahidi kuwaongeza mshara au kuwapandisha cheo. Imekuwa kitu cha kawaida kwa wasichana kutoa rushwa ya ngono ili kupata kazi kwa sasa kazi zimekuwa ngumu sana na isitoshe kuna wanafunzi wengi ambao wanamaliza elimu ya juu na kutegemea kuajiriwa.

      Ø  Utoro na Kutowajibika Ipasavyo;
Hili ndio janga la kitaifa hapa nchini kwetu kwani utoro umekithiri sana ofisini. Wafanyakazi wangine wanakuja ofisini wana saini na kuondoka na wangine muda wa lunch ukifika wakitoka kwenda kula ndio kimoja mapaka kesho. Wafanyakazi hawaishiwi visingizio leo kafiwa na mama mkwe kesho jirani kuna harobaini mara kuna mgonjwa hosipitali unataka kwenda kumuona yaani nivisingizio mwanzo mwisho. Wafanyakazi wangine kutowajibika ipasavyo yani atafanya kazi kidogo muda mwingine wote atalala kwenye meza yake mpaka muda wa kuondoka akiulizwa atadai anaumwa najiskia vibaya.
 
      Ø  Umbea na Dharau kazini;
Siku hizi unaweza kuingia ofisi fulani ukakuta secretary na mwenzie wanamsema mfanyakazi mwenzao hawajali kama wewe upo hapo dirishana unasubiri wakupe huduma uliyofuata au kuapata maelekezo fulani watakuangalia mpaka wamaliza umbea wao ndio wakusikilize shida yako. Kuna baadhi ya wafanyakazi wanajisahau kufanya kilicho waleta nakujikuta wakitumia muda mwingi kuwa sema wafanyakazi wenzao au watu wanaokuja kupata huduma kwenye ofisi hiyo unaweza kukuta mtu hamfahamiani lakini anakuletea dharau kama ulimchukulia mume wake na haswa hizi tabia wanazo sana wanawake hasa wale wanaokaa mapokezi. 
 
      Ø  Mavazi yasiyo faa;
Wafanyakazi wa siku unaweza sema ni kizazi cha swagga kwani wengi wao ni vijana tofauti na zamani mtu anamaliza chuo akiwa mtu mzima lakini sasa ni watoto wadogo tu ndio wanao maliza chuo kwahiyo bado wana akili za ujana wa kuvaa nguo fupi zakubana na kuonesha vifua vyao kwa kuacha kufunga kifungo cha juu na wangine kuvalia suruali chini ya makalio. Wakiulizwa wanakuwa wakali kama mbogo.
 
      Ø  Ulevi, Wizi, Matusi;
Unakuta asubuhi mfanyakazi amekuja ofisini na mning’inio wapombe alizo kunywa jana usiku yani akiongea ananuka pombe utadhani aliamkia bar ndio amekuja kazini. Ofisi zingine unakuta wanaitana majina kwa matusi yani matusi ndio kiunganishi katika maongezi yao au unakuta mteja anatukanwa na kujibiwa hovyo hovyo tu. Ofisi haieleweki yani ukiacha mzigo wako kidogo tu haukuti wafanyakazi wamebeba.
Tubadilike watanzania kwa kuheshimu kazi uliyopata na kuwajibika bila kutaka rushwa na kunyenyekewa kama wewe mfalme kumbuka kuna leo kesho. Tufanye kazi kwa bidii na tupunguze utoro ili tukuze uchumi wa nchi yetu na uchumi wa mtu binafsi.

No comments:

Post a Comment