TTCL

EQUITY

Tuesday, July 2, 2013

TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI.MTU MMOJA AGONGWA NA GARI NA KUFA PAPO HAPO.

Kama ule usemi usemao hatujui yatakayo tokea kesho, ndicho kilichotoa muda mfupi uliopita majira ya saa moja jioni jana tarehe 02/07/2013, baada ya gari dogo lililokuwa linatokea maeneo ya Ubungo kwenda uelekeo wa Buguruni kumgonga mwenda kwa miguu aliyekuwa anavuka barabara katika maeneo gereji (garage) Maeneo haya ni mara baada ya kituo cha daladala mabibo external, kituo kinachofuata kama unakwenda Buguruni kinaitwa gereji, hapa ndipo ilipotokea ajali hiyo

Mtu aliyegongwa hakuweza kufahamika kwa wakati huo na mashuhuda wengi wa ajali hiyo, lakini ni kijana wa kiume mwenye umri kati ya miaka 30 na 22, rangi yake ni mweusi,  na alikuwa amevaa t-shirt nyeupe iliyokuwa na maandishi ya ADIDAS
 
Kwa hakika maisha yetu wanadamu ni mafupi sana!! tunaweza kuwa na mipango mengi na malengo mazuri sana, lakini mwisho wetu ukawa hivi pasipo hata kutarajia!! ndio maana wale wanao amini juu ya maisha mengine baada ya kifo, wanafundisha na kusema tunapaswa kujiweka tayari kiroho wakati wote
 


Damu ilimtoka kwa wingi sana mara baada ya ajali katika maeneo ya kichwani, na hapo ilipotokea ajali kuna kivuko cha waendeo kwa miguu!! kwa mtazamo usio na uthibitisho wa daktari, kijana huyo alifariki muda mfupi baada ya ajali. Tunaomba kuchukua nafasi hii kuwakumbusha madereva wote wazingatie sheria za usalama barabarani, hapa ilipotokea ajali kuna kivuko cha waenda kwa miguu na pia kuna kituo cha mabasi (daladala) kwa vyovyote dereva alitakiwa kupungumza mwendo na hata kama pa mtu anavuka angeweza kumwona na kuepusha ajali. Tunaliomba jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani, wasichoke kuwaelimisha madereva juu ya alama za barabarani

No comments:

Post a Comment