Jeshi lashika nchi; Lasimamisha Katiba
Rais
Mohammed Morsi wa Misri aliyechaguliwa kwa njia za demokrasia
amepinduliwa na jeshi la nchi hiyo na Katiba ya nchi hiyo imesitishwa
huku jeshi likimteua Jaji wa Mahakama ya Katiba kuwa Mkuu wa Muda wa
Nchi. Akizungumza katika televeshini Mkuu wa Jeshi la Nchi hiyo Generali
Abdel Fattah Al-Sisi amesema kuwa jeshi la nchi hiyo haliwezi kuiacha
Misri ikiwa katika hali ya kuyumba na mgongano wa kisiasa usiokwisha na
hivyo ili kulinda maslahi ya watu wa Misri na taifa lao jeshi limeamua
kuchukua nchi. Habari hizo zimesababisha mlipuko wa shangwe kwa maelfu –
kama siyo mamilioni – ya wananchi wa Misri ambao walikuwa wamekusanyika
kwa siku kadhaa sasa katika viwanja vya Tahrir ambao walikuwa
wanasubiria habari hii kwa shauku kubwa.
Gen al-Sisi akizungumza kwenye Televisheni
Wanajeshi wakisimama kulinda Makao Makuu ya Kikosi Maalum cha Ulinzi wa Rais
No comments:
Post a Comment