TTCL

EQUITY

Friday, July 19, 2013

HII NDIO REDIO HABARI MAALUM KUTOKA ARUSHA



Fred Nyman - mwanzilishi wa RHM

Historia ya Redio Habari Maalum

RHM (Redio Habari Maalum) kwa sasa Habari Maalum media. Ni studio inayoshughulika na uandaaji wa vipindi vya Redio ambavyo vinarekodiwa na kurushwa katika Stesheni mbalimbali. Habari Maalum Media iko kilometa kumi na tano (15km) Kaskazini mwa mji wa Arusha barabara iendayo Nairobi kupitia Namanga. Mwanzilishi wa kazi hii ni Mchungaji Fred Nyman kutoka Finland. Lengo kuu la kuanzishwa kwa Redio Habari Maalum ni kuwafikia watu kwa injili, wapatao milioni 70 wanaozungumza kiswahili katika eneo la Afrika mashariki na kati. Maandalizi ya kipindi cha kwanza yalianza kwenye miaka ya sitini. Tarehe 05/09/1976, kipindi cha kwanza cha dakika kumi na tano kilirushwa na FEBA Radio huko Seychelles kupitia masafa mafupi au short wave (SW) na mtangazaji wa kwanza aliyetangaza kipindi hicho alikuwa Mchungaji Fred Nyman wa Finland ambaye kwa sasa ni mchungaji nchini Finland.

Habari Maalum Media

Habari Maalum Media (HMM) ni mojawapo kati ya idara  zilizopo chini ya  kanisa la Free Pentekoste Church of Tanzania (FPCT). Habari Maalum Media tunashughulika na Uandaaji wa vipindi vya Redio na Televisheni ambavyo vinarekodiwa katika studio zetu na kurushwa katika Stesheni mbalimbali za Redio na Television ndani na nje ya Nchi ya Tanzania.Habari Maalum Media tunaendesha kozi mbalimbali kama kozi  za Uandaaji na Utangazaji wa vipindi vya Redio naTelevisheni (MPT) pamoja na kozi za Mazingira. Tunarekodi nyimbo katika Audio na Video kwa kutumia vifaa vya kisasa na kwa ubora wa hali ya juu. Kutokana na studio ya kisasa tuliyonayo na vifaa vya kisasa vya "digital Audio and Video Recording " tunaweza turekodi nyimbo katika Audio na Video kwa ubora wa hali ya juu na kuweza kukupatia wewe nyimbo bora katika CD, Kaseti, kanda za Video (VHS tapes) na DVD.

No comments:

Post a Comment