HAPA NI WAKATI AMBAPO DR KUTOKA HOSPITALI YA WILAYA YA KAHAMA AKIWA AMEINGIA NDANI YA KABURI KUANZA KUKAGUA MWILI WA MAREHEMU LUPIMO LUGENZI (37)
Ama hakika waswahili hawakukosea waliposema
ukistaajabu ya Musa utayaona ya filauni.
Leo katika kijiji cha Ngongwa kata ya Ngongwa
wilayani Kahama Mwili wa marehemu Lupimo Lugenzi(37) umezikwa mara mbili baada
ya Jeshi la Polisi Kuamuru kufukuliwa Mwili huo kwa madai kuwa umezikwa bila
kukaguliwa na Daktari.
Tukio hilo lililojenga taswira ya Pekee
katika kijiji hicho limetokea leo jioni katika kijiji hicho nje kidogo ya mji
wa Kahama.
Marehemu Lugenzi alipata ajari jana majira ya saa mbili usiku maeneo ya
Kanegere Magereza alipogonga tera la Ng’ombe wakati akiendesha pikipiki
iliyokuwa imepakia watu wawili kutoka Ngongwa kuelekea Mwabomba.
Kwa mujibu wa Kaka wa Marehemu Mabala Lugenzi
ameiambia Blog hii kuwa Mara baada ya kupata ajali hiyo walikimbizwa hospitali
ya wilaya ya Kahama lakini Marehemu Lugenzi alifariki dunia njiani kabla ya
kufika Hospitali.
Akiendelea kufafanua Mabala amesema walipoona
mdogo wao ameaga dunia waliamua kumrudisha nyumbani kwa ajili ya Maziko pasipo
kufika kituo cha Polisi wala mwili kuchunguzwa na Daktari.
Akiendelea kufafanua Mabala amesema mara
baada ya kumaliza kuzika na kuweka mashada ya maua walishangaa kuona Polisi
wakiwasili na Daktari na kuwaamuru wafukuwe mwili huo ili ufanyiwe uchunguzi
kwa mujibu wa sheria.
Mara baada ya kukaguliwa Mwili huo na
kujiridhisha kuwa kilichomuua ni ajali waliruhusiwa kumzika upya na hatimaye ndugu na jamaa kuanza
kuweka mashada kwa mara ya Pili.
No comments:
Post a Comment