TTCL

EQUITY

Friday, May 24, 2013

Dar yatanda hofu

Rama mla watu ameachiwa huru

Mtuhumiwa wa kesi ya mauaji Ramadhamani Selemani Mussa, maarufu kama ‘Rama mla kichwa’, aliyekutwa na kichwa cha mtoto kikiwa bado kinavuja damu, pamoja na mama yake Hadija Ally,wakiwa chini ya ukinzi mkali     Dar es Salaam
HATIMAYE mtuhumiwa wa kesi ya mauaji ya mtoto Ramadhamani Selemani Mussa, maarufu kama ‘Rama mla kichwa’, aliyekutwa na kichwa cha mtoto kikiwa bado kinavuja damu, pamoja na mama yake Hadija Ally, wameachiwa huru. 
Rama na mama yake walikuwa wakikabiliwa na shtaka moja la kumuua kwa makusudi mtoto Salome Yohana (3), kinyume cha kifungu cha 196 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA).
Hata hiyo Mahakama Kuu ilimwachia huru Rama baada ya kuridhika na ripoti ya jopo la madaktari waliomfanyia uchunguzi wa Akili zake, iliyoeleza kuwa wakati wa
tukio hilo hakuwa na akili timamu.
Hata hivyo Rama Mla Watu, ataendelea kukaa katika hospitali ya wagonjwa wa akili ya Isanga mkoani Dodoma mpaka akili yake itakapokuwa sawa ndipo ataachiwa kuwa huru mtaani ili asije akawadhuru watu wengine. Khadija Ally yeye ameachiwa huru. Rama alijizolea umaarufu mkubwa mwaka 2008 baada ya kukamatwa akiwa na kichwa cha mtu kinachodaiwa kuwa ni cha mtoto Salome.

No comments:

Post a Comment