Nijeria yapatamachafuko ya vurugu za waasi wa kundila MEND
Wapiganaji nchini Nigeria,
wanaodai kutoka kundi ambalo halijakuwa likiendesha harakati zake tangu
mwaka 2009, wanasema wamefanya shambulio ambalo limewaua polisi 12
Kundi hilo la MEND kutoka eneo la Niger Delta, limesema kuwa lilihusika na uvamizi huo Kusini mwa Nigeria siku ya Ijumaa.Wiki jana ujumbe mwingine kutoka kwa kundi hilo ulisema kuwa,Mend itaanza tena kufanya mashambulizi, baada ya kiongozi wake Henry Okah, kufungwa jela Afrika Kusini.
Polisi walikanusha madai yaliyotolewa Ijumaa kuwa shambulizi hilo lina uhusiano wowote na vitisho vya kundi hilo.
Walisema kuwa ilihusu mgogoro kuhusu malipo yao baada ya maafikiano ya msamaha.
Maelfu ya wapiganaji wa zamani wanastahili kupokea mishahara yao kama sehemu ya makubaliano yaliyoafikiwa ya msamaha kwao.
Hata hivyo, wakati baadhi ya makomanda wameweza kutajirika kutokana na mkataba huo, baadhi ya wapiganaji barobaro, bado hawajapokea malipo yoyote.
Maafisa 12 walisemekana kutoweka, wakihofiwa kufariki baada ya watu waliokuwa wamejihami kushambulia kituo cha polisi katika eneo la Niger Delta.
Mashua iliyokuwa imewabeba polisi takriban 50, waliokuwa wanaelekea katika mazishi ilikwama majini, jambo lililoifanya kuwa rahisi kuweza kuwashambulia.
Kundi la MEND, limekuwa likipigania sehemu ya mafuta kutoka Kusini mwa Nigeria lakini halijakuwa likiendesha harakati zake tangu mwaka 2009 ambapo mkataba wa kusitisha mapigano uliafikiwa.
Okah, ambaye ni kiongozi wake alihukumiwa jela kifungo cha miaka 24 mwezi jana kwa kuongoza mashambulizi ya mabomu mjini, Abuja, mwaka 2010.
Kuanza tena kwa mgogoro katika eneo la Niger Delta kutaathiri pakubwa sekta ya mafuta nchini Nigeria.
No comments:
Post a Comment