NAPE: WANAYOFANYA CHADEMA BUNGENI NI KUWADHIHAKI WANANCHI WALIOWACHAGUA
CHAMA
Cha Mapinduzi (CCM) kimeeleza kukerwa kwake na matukio ya kejeli matusi
na uvunjifu wa amani yanayoanza kushamiri bungeni
na kusema kuwa matukio hayo ni dhihaka ya hali ya juu inayofanywa na wabunge dhidi ya wananchi waliowachagua.
Hayo
yalisemwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi,
Nape Nnauye wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika
kwenye Uwanja wa shule ya Msingi, Gairo mkoani hapa, Aprili 18, 2013,
ambao mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
”
Mambo haya yanayofanywa na wabunge kama ilivyotokea jana (juzi), ni
dhihaka inayofanywa na wabunge kwa wanancjhi waliowachagua. Baadhi ya
wabunge wanafanya vituko hivi huku wakiwa wanatambua wazi kwamba heshima
waliyopewa ni kwenda bungeni kujadili matatizo ya wananchi ambayo ni
mengi kama migogoro ya ardhi. Hili tukio la jana ni aibu ya mwaka”,
alisema Nape.
Alisema,
muda wanaokuwepo bungeni, wabunge wanapaswa kuutumia wote kwa hekima
busara na uwezo wao wote kujadili namna ya kuwezesha Watanzania kufikia
maisha bora na siyo kuutumia muda huo kujadili tofauti zao za kisiasa au
namna ya kutekeleza malengo yao binafsi ya vyama vyao.
”Hatua
hii ya wabunge wa Chadema kuamua kuzusha tafrani na kuvunja kanuni za
bunge kwa makusudi ni ya hatari sana, hivyo wananchi wanapswa kujifunza
kwamba hawa siyo watu wa kuwapa madaraka. Tazama hivi sasa bungeni wapo
wachache sasa wananchi wakihadaika wakawachagua na kuwa wengi bungeni
patakuwaje? Hili ni fundisho tosha”. alisema Nape.
Alisema,
hatua ya Wabunge na viongozi wa Chadema kulijadili suala la Mkurugenzi
wa Usalama wa Chama hicho, Wilfred Lwakatare kuhusiana na ugaidi huku
wakijua kwamba ni suala ambalo lipo mahakamani, ni la kujaribu kuingilia
uhuru wa mahakama kwa makusudi ili ifikie mahala mahakama itupilia
mbali kesi hiyo kwa kigezo cha kuinngiliwa uhuru wake.
”Haya
ni matumzi mabaya ya bunge ambayo yanasukumwa na viongozi wao ikiwemo
kuingilia uhuru wa mahakama, ili hatimaye ionekane uhuru wa mahakama
umengiliwa kuhusiana na kesi hiyo na hatimaye itupiliwe mbali. Kila
mwenye akili anajua kwamba huu ni mkakati malum wa Chadema”, alisema
Nape
Mbali
na kukizungumzia bungeni suala ya Lwakatare, Chadema wamekuwa
wakilisema pia mitaani, akitoa mfano hatua ya hivi karibu ya Mbunge wa
Singida, Tuntu Lissu kufanya mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia
suala hilo na kwamba mbali na kutafuta kesi hiyo itupwe pia ni juhudi za
Chadema kujaribu kusukuma maamuzi ya mahakama.
”Inashangaza
sana, Lisu badala ya kutoa ushahidi wake maghakamani kuhusu suala hili
anakwenda kujzungumza na wandishi wa habari ili hali anafahamu wazi
kwamba kesi kuhusiana na suala hilo ipi mahakamani, tafsiri yake ni
kwamba ni juhufdi za Chadema kujaribu kusukuma maamuzi ya mahakama au
kushawishi mahakama kutupilia mbali kesi kwa kigezo kwamna imeingiliwa
uhuru wake”, alisema na kuongeza:.
”Mbowe
(Mwenyekiti wa Chadema, Freman Mbowe) pia wakati akizungumza Bungeni
alitumia muda mrefu kuzungumzia suala la Lwakatare lililopo mahakamani.
leo mahakama ionekane uhuru wake umeingiliwa iitupe kesi, na hata wakati
wa kuchangia bajeti ya Utumishi, upande wa Chadema badala ya
kuzungumzia sekta ya utumishi wa umma kurasa nne nzima zilihusu mambo ya
Lwakatare”, huu ni mkakati mbaya sana unaolenga haki isitendeke kuhusu
kesi hiyo.
Akizungumzia
hatua ya Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema kutamka bungeni kwamba
CCM Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete na Chama Chake cha CCM ndiyo
chanzo cha udini, aling’aka kwamba ni kauli inayotia shaka uelewa wa
mambo wa mbunge huyo.
”Nina
mashaka kama Lema ni mzima kiakili, CCM italetaje udini wakati ndiyo
imeleta umoja na mshikamano kwa makabila zaidi ya 24 ya Tanzania kiasi
kwamba amani na utulivu vimeshamiri? Yaani CCM ihangaike kujenga
mshikamano halafu hiyo hiyo ione kicefuchefu kuilinda na kuanza
kuihujumu? huu ni upuuzi wa hali ya juu sana”, alisema Nape.
Nape
alisema, vituko vyote vinavyoendelezwa na Chadema Bungeni na kwingineko
ni dalili tisha kwamba wanaendelea kutekeleza ahadi waliyotangaza siku
nyingi kwamba nchi haitatawalika.
Mkutano
huo ulifanyika ikiwa ni sehemu ya ziara ya Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana inayoendelea mkoani Morogoro, ambapo pamoja na Nape,
Kinana anafuatana na Katibu wa NEC, Oganaizesheni Mohamed Seif Khatib.
Ni ziara ya kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa ilani ya CCM mkoani
humo.
No comments:
Post a Comment