Dodoma,Tanzania
WAKATI Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema (Chadema) akiachiwa kwa
dhamana jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha,kufuatia kesi ya
uchochezi inayomkabili, wiki hii Lema anaweza kukutana na rungu la Spika
wa Bunge Anne Makinda endapo atashindwa kudhibitisha kauli aliyowai
kuitoa Bungeni kwamba Rais Jakaya Kikwete ni mdini.
Akizungumza Bungeni April 17 mwaka huu kwa mara ya kwanza tangu
alipotoka likizo ndefu kama anavyopenda kuita, Lema alianza kwa kusema,
Mh. Naibu Spika mimi nahofia kung'olewa kucha zangu, kope zangu,meno
yangu na macho yangu", Lema pia alisema kwamba Rais Kikwete amekuwa
mwasisi wa udini nchini Tanzania na kusababisha chanzo cha vurugu za
udini.
Hata hivyo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu
na Bunge, William Lukuvi aliomba mwongozo wa Spika na kudai kwamba Lema
amemdhihaki Rais Kikwete na kumtaka akanushe kauli yake kwanza, kwa
sababu kanuni za bunge haziruhusu jina la rai kutumika kwa dhihaka.
Naibu Spika Job Ndugai alimtaka lema kukanusha kauli yake hata
hivyo Lema hakufanya hivyo, badala yake akasisitiza kwamba hakuna cha
kukanusha kwa sababu Rais Kikwete ndiyo mwasisi wa vurugu za udini
nchini Tanzania.
"Mh. Spika mimi sioni cha kukanusha hapo, kwa sababu
sijamdhihaki Rais bali nilichokisema ni kusisitiza kwamba yeye ndiye
mwasisi wa udini nchini" baada ya kauli hiyo Lema aliendelea kutetea
hoja yake lakini dakika moja baadaye Mwanasheria Mkuu Frederick Mwita Werema alisimama na kumtaka Lema adhibitishe kauli yake ama akanushe.
Baada
ya Mwanasheria Mkuu kusimama Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni
Tundu Lissu pia akasimama na kusema kwamba Lema hajamdhihaki Rais bali
ametumia maneno makali juu ya rais ambayo yanaruhusiwa kwa muujibu wa
kanuni za Bunge hilo huku akifafanua kwamba dhihaka ni utani na kwa
mantiki hiyo ndani ya bunge hili hakuna utani bali kuna mambo ya msingi.
Lissu akiwa mtu wa tatu kuzungumzia hoja hiyo ya Lema,
Mwanasheria Mkuu akasimama tena na kusema kwamba tafsiri ya neno dhihaka
ni udini hivyo Lema bado anahitaji kudhibitisha kauli yake, Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais, Sera na Uratibu, Steven Wasira alikuwa mtu wanne
kuzungumzia hoja ya Lema baada ya lema kumtaja kwamba alishindwa
kutatua vurugu za kuchinja kule Mjini Mwanza pamoja na Geita.
Wasira alilazimika kusimama kutetea hoja hiyo huku akidai
kwamba hakushindwa bali aliwataka viongozi wa dini kutatua suala hilo na
kuwataka watizame njia sahihi ya kuishauri serikali, kauli iliyopingwa
na lema kwa madai kwamba huo ni udhaifu wa serikali na uonga wa kufanya
maamuzi magumu kwa maslahi ya Taifa.
Baada ya mjadala huo, Naibu Spika Job Ndugai alimtaka Lema
kudhibisha kauli yake ndani ya wiki moja, hata hivyo siku moja baadaye
Mbunge huyo na wezake wanne wakaondolewa Bungeni baada ya kukataa amri
ya Naibu Spika huyo kuamuru Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu
atolewe nje ya ukumbi kwa kosa la kuomba mwongozo zaidi ya mara 10, hata
hivyo kabla ya Lema kurudi bungeni akakutana na balaa la Mkuu wa Mkoa
wa Arusha Magesa Mulongo.
No comments:
Post a Comment