FAHAMU UKWELI KUHUSU MWIGIZAJI NA MCHEKESHEJI WA KUNDI LA VITUKO SHOW MAARUFU KWAJINA LA MASAI NYOTA MBOFU
Bw. Gilliady Severine (Masai Nyota mbofu)
sanaa nilianza mwaka 1998 nikwa nachekesha watu mtaani na kuiga sauti za watu maarufu miongoni mwao ni msanii nguli wa vichekesho hapa nchini Tanzania Dikson Makwaya maarufu kwa jina la BAMBO mpaka baadhi ya mashabiki mtaani wakawa wananiita small Bambo kutokana na ubunifu na kuimudu kwa sauti hiyo
Siku moja nikakutana na Bambo mwenyewe live katika tamasha moja la kidini lililofanyika mjini Arusha lililofanyika katika ukumbi wa sinema unaofahamika kama METRAL POP nikamwomba bambo nafasi ya kuperform naye akanikubalia basi watu wakashangilia sana ndipo bambo akaniachia mawasiliano yake baada ya hapo nikawa na tembea nae katika matamasha mbali mbali na nikajiunga na kundi linalojulikana kama MAHOKA ambapolilikuwa na wanachama kama vile mimi mwenyewe, Mtanga, Bambo, Kingwendu nawengine wengi tu
MASHINDANO MBALI MBALI NILIYOSHIRIKI
Nilifanikiwa kushiriki mashindano mbali mbali yanayohusu industry ya comedy hapa nchi kama vile comedy search iliyoandaliwa na kampuni ya EATV miaka kadhaa iliyopita ambapo nilitoka katika round ya pili na washindi waliopatika ni Bambo, Dr Rushwa, Mtanga, Masawe mtata,Masterface na Kiwewe ambao wanaunda kundi zima la Ze comedy show
pia nilishiriki shindano la kutafuta mkali wa kuchekesha mkoa wa Kilimanjaro shindano hili liliandaliwa na radio ya mjini moshi inayojulikana kama Kill fm ambapo mimi niliibuka kuwa ndio mshindi wa mkoa mzima wa kilimanjaro
Tangu hapo ndi ukawa mwisho wangu wa kuvaa vichupi na kuchekesha mabarabarani na kwenye mabaa bali nikawa naitwa kwenye harusi na sherehe mbali mbali
KUANZA KWANGU KUONEKANA RUNINGANI
Nilianza kuonekana kwenye runinga baada ya kujiunga na kikundi cha Jakaya theator lililokuwa linarusha tamthilia yake kupitia ITV kwa muda wa miezi tisa [9] ambapo baada ya hapo Mungu akanisaidia nikaingia mkataba na kampuni niliyopo sasa AL-RIYAMY PRODUCTION ambapo sasa tuna kipindi chetu pale channel ten kila alhamis saa tatu usiku kupitia kampun hii ya AL-RIYAMY PRODUCTION
No comments:
Post a Comment