TTCL

EQUITY

Friday, February 22, 2013

Jimbo la Kaskazini Mashariki lapambana na changamoto za utendaji mbaya wa elimu


Maafisa wa elimu wa Jimbo la Kaskazini Mashariki ya Kenya wanasema wameshangazwa na utendaji mbovu katika mitihani ya Cheti cha Elimu ya Msingi (KCPE) mwaka 2012.
  • Wanafunzi wa shule ya msingi wakisoma katika darasa tupu. Jimbo la Kasjkazini Mashariki la Kenya lilikuwa la chini kabisa nchini katika mitihani ya Cheti cha Elimu ya Msingi ya mwaka 2012. [Na Simon Maina/AFP] Wanafunzi wa shule ya msingi wakisoma katika darasa tupu. Jimbo la Kasjkazini Mashariki la Kenya lilikuwa la chini kabisa nchini katika mitihani ya Cheti cha Elimu ya Msingi ya mwaka 2012. [Na Simon Maina/AFP]
"Wazazi, walimu, wafanyakazi, viongozi na wanafunzi wamefanya kila kitu na walikuwa na matumaini makubwa kuwa wangefanya vizuri kuliko miaka iliyopita," Mweka Hazina wa Jumuiya ya Wakuu wa Shule za Msingi (KEPSHA) Ibrahim Boya aliiambia Sabahi.
"Wakati matokeo yaliyotolewa tarehe 28 Januari, wilaya za Garissa, Wajir na Mandera zilikuwa za chini kabisa miongoni mwa wilaya 47 nchini," alisema. "Tulihisi juhudi zetu zilikuwa za bure."
Wilaya ya Mandera ilikuwa ya mwisho nchini ikiwa na wastani wa alama 182 kati ya 500. Wiliya ya Kirinyaga katika Jimbo la Kati ilikuwa ya kwanza kitaifa kwa kupata wastani wa alama 273.
Boya, ambaye pia ni mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi ya Furaha huko Wajir, alisema maafisa wa elimu wa eneo hilo walitarajia wilaya za jimbo ziwe mongoni mwa wilaya zilizofanya vizuri.

Utendaji mbaya unavunja moyo

Wanafunzi wa Kenya wanatakiwa kufanya mtihani wa KCPE baada ya mwisho wa darasa la nane na wanatakiwa wapate angalau alama 200 ili kuendelea na shule ya sekondari.
Mohammed Hashim Abdi, ambaye mtoto wake alifanya mtihani wa mwaka jana katika Shule ya Msingi ya Sala huko Mandera, alisema alihisi kuwa miaka minane ya mtoto wake aliyoitumia kusoma ilikuwa ni kupoteza wakati. Shule ilikuwa ya mwisho kwa kuwa na wastani wa alama 120.
"Mtoto wangu alipata alama 102 katika 500 na hakuna vyovyote shule ya sekondari yoyote inaweza kumpokea," aliiambia Sabahi. "Kinachoniuma mimi ni kwamba maafisa wa serikali kijijini kwangu walinishawishi kumpeleka mwanangu shule ili kuelimishwa badala ya kuchunga mbuzi wa familia."
Matokeo kama hayo yatawavunja moyo wazazi wengi wachungaji ambao wamejitolea sana kuwapeleka watoto wao shule, alisema.
Afisa wa Elimu wa Wilaya ya Garissa Adan Sheikh Abdullahi aliiambia Sabahi mambo mengi yamechangia kwa utendaji huo mbaya wa jimbo, ikiwa ni pamoja na mazingira mabaya ya kujifunzia na kukosekana kwa usalama.
Abdullahi alisema kuwa wadau wa elimu wa Garissa wamepitia utendaji na kukubali kwa pamoja kuchukua dhamana kwa hali hiyo.
"Tuna matumaini kwa kuwa na serikali mpya za wilaya zitakazoanza kazi baada ya uchaguzi wa tarehe 4 Machi, hakuna kitakachoachwa ili kuhakikisha kuwa mkoa unashindana kwa ufanisi na sehemu nyengine za nchi," alisema.
Serikali mpya zinaweza kuajiri moja kwa moja walimu wake wenyewe na kuimarisha sehemu za kusomea bila ya kutegemea seriklai kuu kufanya kazi hiyo, alisema.
"Tunazo hali ambapo shule zenye wanafunzi zaidi ya 600 zina walimu watatu," alisema. Walimu hao hao wanalazimika kujaza pengo na kufundisha masomo ambaayo hawana utaalamu nayo, ili kusaidia tu."

Changamoto ya kuimarisha viwango vya elimu

Licha ya kutoridhika, wakaazi hawatapeleka malalamiko yao kwa Baraza la Mtihani la Taifa la Kenya au kusahihishwa upya kwa karatasi, Boya alisema. Badala yake, walimu, wazazi, maafisa wa elimu na maafisa wa elimu na viongozi wa serikali watachukulia matokeo haya kama changamoto ili kuboresha viwango vya elimu katika jimbo.
KEPSHA imeanza mafunzo ya ujengaji uwezo kwa walimu, hasa katika utoaji wa mitaala, alisema.
"Tuligundua kuwa baadhi ya shule hawakamilishi mitaala yao na pia tutaangalia njia za kuboresha mbinu za kufundishia ili walimu na wanafunzi wafurahie [wanayofanya]," alisema.
KEPSHA inaomba fedha kutoka mashirika ya misaada na Mfuko wa Maendeleo wa Maeneo ya Bunge ili kuendesha mafunzo wakati wa mapumziko ya mwezi mmoja hapo Aprili, Boya alisema. Mafunzo hayo ni mpango elekezi ambao utaanza katika wilaya ya Wajir na baadaye utaanzishwa katika eneo zima.
Mohamud Abdi Mohammed, mgombea wa ugavana wa wilaya ya Wajir, aliiambia Sabahi kuwa ili kuimarisha elimu kwa ufanisi katika eneo hilo, serikali ya mtaa itashughulikia masuala yaliyopo ambayo yanaathiri uwezo wa familia kuwapeleka watoto wao shule.
"Tutahitaji kujenga nyumba zaidi za kulala wanafunzi ili kuwaweka wanafunzi ambao familia zao zinahamahama na mifugo yao," alisema. "Tutashughulikia pia masuala ya usalama wa chakula na uhaba wa maji mambo ambayo yatahakikisha kuwa mpangilio wa masomo haukatishwi."

No comments:

Post a Comment