DODOMA: Jeshi la Polisi nchini, limemtia mbaroni Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu na kumsafirisha kwenda jijini Dar es Salaam kwa tuhuma ambazo hazikuwekwa wazi.
Lissu ambaye pia ni mwanasheria mkuu wa Chadema amekamatwa leo saa 12:10 jioni wakati akitoka nje ya eneo la ukumbi wa Bunge.
Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe
amethibitishia gazeti hili kwa njia ya simu juu ya kukamatwa kwa
mbunge huyo lakini akasema bado hawajajua sababu za kukamatwa kwake.
“Ni kweli nimepata taarifa kuwa wamemkamata kama dakika 20
zilizopita (saa 12:10) na sasa hivi wako njiani kumpeleka Dar es Salaam.
Sasa sijui anapelekwa kituo cha kati au wapi,” alisema.
“Hatujajua kama pia anapelekwa kule kwenye kikosi kazi ama
Central Police (kituo cha kati) lakini ninachoweza kusema ni kweli
amekamatwa na Polisi. Sina taarifa zaidi,” alisisitiza Mbowe.
No comments:
Post a Comment