Nina kila sababu ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa wema wake,
kwa kunipa na kukupa nafasi wewe msomaji wangu kujumuika nami katika
kuelimishana juu ya maisha ya mapenzi kupitia safu hii murua ya life & stlyle
Mada ya leo inazungumzia wale ambao waliamini au wanaamini kuwa ndoa ni
jambo la kawaida.
Yaani waliamini au wanaamini ni kama kwenda kununua nguo dukani
Kariakoo kisha kuijaribisha na kuivaa. Lakini fasheni yake ikipita basi
wanaitupa au kuigawa.
Rafiki, ndoa siyo hivyo. Ndoa ni mkataba wa maisha, mkataba wa kudumu
na kuvumiliana kwenye shida na raha.Uzuri wa mapenzi bwana,
ukishaingia, umeingia, haijalishi uliingia kwa mtindo upi, kitu
kikishakukolea hata ufanyeje.
Kwa leo napenda kuwashauri ambao wako nje ya ndoa kuwa ndoa siyo nguo
useme unaweza kuinunua, ukaijaribisha au ukaivaa na baadaye ukaiacha.
Ndoa ni kiapo, tena kiapo cha kifo, kwani mkishaungana ili kutengana
basi ni hadi pale Mola atakapomtwaa mmoja wenu.
Ingawa inawezekana kiapo hicho ni tofauti kwa imani nyingine, lakini
sehemu kubwa ndoa ni muunganiko wa jinsi mbili tofauti ambazo zinaungana
na kuwa mwili mmoja. Jambo lako ndiyo la mkeo, la mumeo ndiyo lako,
hiyo ndiyo maana ya ndoa kisha ndipo yanafuatia mambo mengine kama
kusaidiana, mambo ya kawaida na hata yale ya kimapenzi.
Ushauri wangu kwako ambaye bado hujaoa/ kuolewa ni kuwa makini sana
na uchaguzi wako. Hapa ‘kinachomata’ ni kuwa makini sana na mtu ambaye
unataka kuingia naye kwenye kiapo cha maisha yako. Usikurupuke kwa
sababu labda jamaa anaonekana ni ‘hendsam’, achana na uzuri wake, weka
pembeni hilo gari lake alilokuja nalo kukupigia misele mtaani au
nyumbani kwenu.
Kwanza inawezekana aliazima kwa washkaji zake, dada’ke, kaka’ke,
shemeji yake au amekodi ilimradi tu akuweke roho juu. Achana na kazi au
elimu nzuri aliyonayo, mwanaume au mwanamke wa ndoa hachaguliwi kwa
mtindo huo, hachaguliwi kwa kuangalia vigezo hivyo bali ni lazima
ujiridhishe kama je, ana vile vitu unavyovihitaji katika maisha yako?
Kama hana, basi huyo hakufai maana itafika sehemu unamuacha au
utamtafutia sababu za hapa na pale ili muachane.
Kwa mfano, unapenda mwanamke au mwanaume ambaye ni mpole, basi tafuta
mwanaume mwenye hulka na tabia hizo ili uishi katika ndoa ambayo
unaipenda. Lakini ukiolewa ilimradi umeolewa nakwambia
itakugharimubaadaye.
Vijana wengi wa sasa wanachagua watu wa kuishi nao kama wanandoa kwa
sababu ya kitu f’lani ndiyo maana baada ya muda f’lani unasikia ile ndoa
ambayo ilivunja rekodi mjini au kijijini, imevunjika, ukichunguza kwa
undani utagundua kuwa sababu ni kile kilichowaunganisha ambacho sasa
kinakuwa kimeisha au hakipo.
Kwa ushauri wa mambo mbalimbali ikiwemo elimu ya uzazi, ndoa na mahusiano, aidha maoni tembelea ukurasa wetu wa Sweetness of affection
No comments:
Post a Comment