TTCL

EQUITY

Saturday, April 16, 2016

Vijana watakiwa kuacha kuchagua kazi za kufanya

Serikali imeandaa programu ya kuwasaidia vijana kupitia makundi mbalimbali hasa ya uzalishaji mali.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na walemavu mheshimiwa Anthony Mavunde amesema vijana na nguvu kazi inayoingia kwenye ajira ni takribani watu laki 8 mpaka milioni moja kwa mwaka na hali hiyo husababisha kundi kubwa la watu ambao hawapati nafasi za moja kwa moja kujiingiza kwenye shughuli mbalimbali.
Akizungumza na East Africa TV leo jijini Dar es salaam Mavunde amesema serikali imeandaa programu ya kuwasaidia vijana kupitia makundi mbalimbali hasa ya uzalishaji mali.
Amesema utaratibu uliowekwa sasa pamoja na kuwatambua na kuwalasimisha rasmi nikuona jinsi ambavyo wanaweza kuwezeshwa ili kuweza kukidhi mahitaji yao kwa sababu wengi wanaolalamikia ajira ni wale ambao wako tayari kufanya shughuli za ujasiliamali lakini wanachangamoto ya kupata mitaji na mikopo.
Mavunde ameongeza serikali haitasita kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaojihusisha na ufujaji wa fedha za serikali ambazo zinatolewa kwa ajili ya kuendeleza makundi maalumu nchini lengo ikiwa ni kuhakikisha nchi inaingia katika uchumi wa kati.

No comments:

Post a Comment