TBL Group yawapiga msasa kuhusiana na changamoto za ajira
Taasisi
na makampuni mbalimbali mwishoni mwa wiki yalishiriki katika semina ya
kuwaandaa wanafunzi wanaosoma vyuo vikuu kuingia kwenye ajira
watakapomalizika masomo yao ambayo ilifanyika katika Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam na kushirikisha wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali vya elimu ya
juu.
Kampuni
ya TBL Group ilishiriki katika semina hiyo ambapo Meneja wake wa
kuendeleza vipaji Lilian Makau,alitoa mada kuhusiana na jinsi ya
kuhimili kufanya kazi kwenye kampuni kubwa na zenye mifumo thabiti ya
kiutendaji na changamoto za kupata ajira.
Wanafunzi
wengi pia walipata fursa ya kuuliza maswali mbalimbali kuhusu taratibu
za ajira katika kampuni ya TBL ambapo aliwaeleza kuwa kampuni inatoa
fursa za ajira kwa watanzania wote na taratibu zake za ajira ziko wazi
na pia kuwa imekuwa na utaratibu wa kuajiri wasomi waliohitimu mafunzo
vyuoni na kuwapatia mafunzo ya ndani na wengi wao wametokea kuwa na
utaalamu wa kiwango cha juu baada ya muda mfupi kwenye ajira zao.
Meneja
wa kuendeleza vipaji wa TBL Group, Lilian Makau akitoa mada wakati wa
semina ya kuwaandaa wanafunzi wanaosoma vyuo vikuu (hawapo pichani)
kuingia kwenye ajira watakapomalizika masomo yao iliyofanyika jijini Dar
es Salaam.
Pichani juu na chini ni baadhi ya wanafunzi wakisikiliza mada na kuuliza maswali.
Baadhi
ya wanafunzi wakipata maelekezo kutoka kwa Meneja wa kuendeleza vipaji
wa TBL Group, Lilian Makau muda mfupi baada ya kumalizika semina.
No comments:
Post a Comment