Na Nathaniel Limu, Singida
Mhasibu
wa Halmashauri ya wilaya ya Singida na mkazi wa Utemini mjini hapa,
Imani Abdul Nyamangaro (44), amepandishwa kizimbani katika mahakama ya
hakimu mkazi akikabiliwa na makosa 57 ya wizi wa mishahara hewa yenye
jumla ya thamani ya shilingi 29,418,642.
Mapema
mwendesha mashitaka wakili wa serikali Michael Lucas Ng’hoboko, alidai
mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Joyce Minde, kuwa kati ya Aprili,29
mwaka 2013 na Machi, 27 mwaka 2014, mshitakiwa Nyamangaro kwa makusudi
aliiba mishahara hewa ya zaidi ya shilingi 29.4 milioni huku akijua wazi
kitendo hicho ni kinyume na sheria.
Ng’hoboko
alisema kuwa mshitakiwa alikuwa akijipatia mishahara hiyo ambayo
wahusika waliisha staahafu kazi muda mrefu,kupitia akaunti yake
no.50802503513 ya tawi la NMB mjini Singida.
Mshitakiwa Nyamangaro alikana kutenda makosa hayo 57 na kesi yake imeahirishwa hadi Aprili, 27 mwaka huu itakapotajwa tena.
Hakimu
wa mahakama hiyo, Minde alisema dhamana ya mshitakiwa ipo wazi na
kwamba atapashwa kutoa shilingi 14,709,321. taslimu mahakamani au awe na
mali isiyohamishika yenye thamani inayolingana na kiasi hicho cha
fedha.
Hadi mwandishi wa habari hizi anaondoka mahakamani hapo, mshitakiwa alikuwa bado hajatekeleza masharti ya dhamana.
No comments:
Post a Comment