Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) imefanikiwa kukamata bidhaa za magendo kwenye
maeneo mbalimbali yaUkanda wa wa Bahari ya Hindi, Ziwa Viktoria na
mipaka mingineyo nchini.
Taarifa
hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi
(TRA) Bw. Richard Kayombo wakati akifanya mahojiano na Mwandishi wa
Idara ya Habari (MAELEZO) Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam kuhusu
juhudi za operesheni ya kutokomeza bidhaa za magendo nchini.
Bw.
Kayombo ameeleza kuwa, katika Mkoa wa Lindi TRA imefanikiwa
kukamatamashua katika bandari ya Lindi ambayo ilisheheni bidhaa za
magendo zenye thamani ya shilingi 159,361,046.
Ameongeza
kuwa katika operesheni hiyo, TRA imefanikiwa kukusanya kodi ya jumla ya
shilingi 10,500,678 kutoka katika bidhaa zilizokuwa katika nyaraka za
forodha (manifest) ambapo pia inategemea kukusanya kodi ya shilingi
19,529,500 kutoka katika bidhaa ambazo zilikuwa katika nyaraka za
forodha lakini thamani yake ilikuwa chini ya beo halisi.
Akitaja
bidhaa hizo za magendo zilizokamatwa katika mashua hiyo ni mifuko 3,725
ya sukari yenye thamani ya shilingi 127,070,562, betri katoni 50,
mchele mifuko 3,087, mafuta ya kula madumu 80, majokofu manne ya mtumba,
baiskeli za mitumbo nne pamoja na katoni 20 za hamira.
‘’Mashua
hiyo ilikamatwa katika bandari ya Lindi tarehe Mosi Februari, 2016
baada ya wasamaria wema kutoa taarifa ya kuwepo bidhaa za magendo ndani
ya mashua hiyo ambapo upakuaji wa shehena hiyo ulianza mara moja’’,
alisema Kayombo.
Kayombo
kaongeza kuwa kwa upande wa jijini la Dar es Salaam, TRA kwa
kushirikiana na Kikosi cha doria cha Jeshi la Wanamaji wameweza kukamata
Jahazi lenye jina la ‘Takbiri’ lenye usajili wa namba Z-875 likiwa
limesheheni lita 19,700 za dizeli ambapo thamani yake bado haijapatikana
kwakuwa imepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili ya Uchunguzi
zaidi.
Aidha,
majahazi mengine matatu yamekamatwa katika eneo la Kigombe mkoani Tanga
ambayo yalikuwa na bidhaa za magendo yenye thamani ya shilingi 99, 682,
273, 48 ambamo ndani kulikuwa na magunia ya sukari, mchele, mafuta ya
kula, matairi ya magari, nyaya za kuzuia mbu, jokofu, jiko la umeme,
rangi za kupuliza, betri na biskuti ambapo majahazi hayo yalitaifishwa
baada ya wahusika kujitosa ndani ya maji na kutoroka.
Aidha,
TRA kwa kushirkiana na Jeshi la Polisi metoa wito kwa umma kuwa
inafanya doria saa 24 kila siku katika maeneo yote yaliyoshamiri
upitishaji wa bidhaa za magendo ambapo imeunda Kanda Maalum katika
maeneo ya Mbweni, Msasani, Kunduchi pamoja na Kigamboni.
No comments:
Post a Comment