Kijana
wa Kitanzania Joseph Stanford ambaye ametembea kwa miguu kutoka Mwanza
hadi jijini Dar es salaam akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani
kuhusu nia yake ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi yake nzuri kwa wananchi.
Kijana
wa Kitanzania Joseph Stanford ambaye ametembea kwa miguu kutoka Mwanza
hadi jijini Dar es salaam akiwaonyesha waandishi wa habari hawapo
pichani mahali alipoanzia kutembea kwa mguu kwa ajili ya kumpongeza Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi
yake nzuri kwa wananchi.
Kijana
Joseph Stanford kutoka Mabatini wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza
amempongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe
Magufuli kwa utendaji wake wa kazi ambapo ametembea kutoka Mwanza hadi
Dar es salaam kwa muda wa siku 25.
Kijana
huyo alianza safari yake jijini Mwanza Januari, 16 mwaka 2016 saa
10:00 alfajiri na ambapo safari hiyo ameihitimisha jijini Dar es salaam
Februari 9, 2016 jioni.
“Matembezi
yangu ni ya hiari na lengo la kutembea huku ni kumpongeza na kumuunga
mkono Rais Magufuli juu ya utendaji wake wa kazi anaoufanya na pia
kumshukuru kwa kuunda Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo”
aliongeza Joseph.
Hata
hivyo, kijana Joseph alisema kuwa katika matembezi yake alikumbana na
changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa wadhamini katika kufanikisha safari
yake ya kumpongeza Rais Magufuli.
Kwa
upande wake Wizira wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye
amesema kuwa anatambua uwepo wa kijana huyo na amempongeza kwa hatua
hiyo ya kishujaa aliyoionesha.
Mbali
na hayo, Kijana huyo ameomba kuwezeshwa kukutana na Rais mstaafu Jakaya
Kikwete ili kumshukuru kwa kuthamini na kuibua vipaji vya vijana
nchini.
Joseph
anaumri wa miaka 20 na pia ni muhitimu wa kidato cha nne mwaka 2015
katika shule ya Sekondari Mtoni iliyopo jijini Mwanza.
No comments:
Post a Comment