NECTA yatangaza matokeo ya kidato cha 4 ufaulu washuka
Akitangaza
matokeo hayo Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la TANZANIA –NECTA,
Dkt. CHARLES MSONDE amesema wasichana waliofaulu ni laki moja thelathini
na moja 913 sawa na asilimia 64.84 wakati wavulana waliofaulu ni laki
moja arobaini na moja elfu na 34 sawa na asilimia 71.09
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la TANZANIA –NECTA, Dkt. Charles Msonde.
Dkt. MSONDE amesema kiwango cha juu cha ufaulu ni kwa somo
la Kiswahili ambapo asilimia 77.63 ya watahiniwa wamefaulu huku kiwango
cha chini cha ufaulu kikiwa ni somo la Hisabati ambapo asilimia 16.76
wamefaulu mtihani huo.
Dkt. MSONDE amesema baraza la mitihani la TANZANIA limeamua kurejesha
mfumo wa madaraja kufuatia maoni ya wadau yaliyoonyesha kuwa wengi wao
hawana uelewa kuhusu mfumo wa viwango.
Katika matokeo hayo shule kumi bora ni KAIZIREGE mkoani KAGERA, Shule
ya sekondari ya wasichana ya ALLIANCE, mkoani MWANZA, Shule ya
sekondari ya wasichana na Saint FRANCIS, MBEYA, Shule ya sekondari ya
wavulana ya ALLIANCE, MWANZA, Shule ya sekondari ya wasichana ya
CANOSSA, DSM,Shule ya sekondari ya wavulana ya MARIAN, PWANI, shule ya
sekondari ALLIANC ROCK ARMY mkoani MWANZA,Shule ya sekondari ya
wasichana ya FEZA, jijini DSM, shule ya sekondari ya wavulana FEZA ya
jijini DSM na URU SEMINARY iliyoko mkoani KILIMANJARO.
No comments:
Post a Comment