TTCL

EQUITY

Thursday, January 7, 2016

Watanzania wamtegemea Samatta Tuzo za Afrika

Macho na Masikio ya watanzania yako Nigeria ambako tuzo ya Mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani inatolewa leo huku Straika wa Tanzania na TP Mazembe akipewa nafasi kubwa ya kuwa Mtanzania wa kwanza kushinda tuzo hiyo kubwa barani Afrika.
 
Macho na Masikio ya watanzania yako Nigeria ambako tuzo ya Mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani inatolewa leo huku Staraika wa Tanzania na TP Mazembe akipewa nafasi kubwa ya kuandika historia ya kuwa Mtanzania wa kwanza kushinda tuzo hiyo barani Afrika.
Samatta ambaye yupo Nigeria kwa sasa akisubiri sherehe za tuzo hiyo, aliondoka nchini hapo jana kuelekea Abuja akiambatana na katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini TFF Mwesigwa Celestine.
Samatta ambaye anatarajiwa kusajiliwa na klabu ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji ameingia kwenye kinyang'anyiro hicho kutokana na mabao yake kuipa TP Mazembe taji la Ligi kuu ya Mabingwa Afrika hapo mwaka jana.
Samatta ambaye aliibuka mfungaji bora wa Ligi ya Mabigwa Afrika akifungana na Staa wa El Marreikh Bakri Almadina kwa mabao saba atachuana na mchezaji mwenzake wa TP Mazembe Robert Kidiaba na Straika wa Etoile de Sahel ya nchini Tunisia Mualgeria Baghdad Bounedjah.
Mshindi wa tuzo hiyo ataamuliwa kwa kura zitakazopigwa na makocha pamoja na wakurugenzi wa ufundi wa nchi wanachama wa shikirikisho la mpira wa miguu Afrika (CAF).

No comments:

Post a Comment