Waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa
Majaliwa,amesema imeweka msisitizo katika kuhakikisha inarudisha nidhamu
kwa watumishi wa uma kwa kuweka mkazo katika uadilifu, uwajibikaji,
kutoa huduma kwa wakati.
Waziri
mkuu Majaliwa ameyasema hayo mkutano wa pili kikao cha tatu Bungeni
Mjini Dodoma alipokua akihitimisha hoja ya kujadili hotuba ya Rais John
Magufuli aliyoitoa siku ya ufunguzi wa Bunge la kumi na moja tarehe 20
Novemba 2015 na kuongeza kuwa serikali itakua inawakumbusha watanzania
na watendaji wa serikali wanafanya majukumu yao kwa wakati ikiwa ni
pamoja na kuchukua hatua za haraka dhidi ya watumishi wanaokwenda
kinyume na misingi ya utendaji kazi serikali kwa kuzingatia kauli mbiu
ya hapa kazi tuu.
Amesema kuwa baadhi ya hoja zilizotolewa na wabunge ambazo utekelezaji wake utahitaji kutengewa fedha za uandalizi wa kutenga fedha za serikali na utendaji wake utafanyika kwa haraka kwa kuzingatia maombi na hoja za wabunge kwakusimamia mapato ya Taifa yanaongezeka kwa kiwango kikubwa.

No comments:
Post a Comment