TTCL

EQUITY

Tuesday, January 12, 2016

SHAURI LA MGOMBEA UBUNGE ILEMELA LAFUTWA

Mahakama kuu kanda ya Mwanza limefuta rasmi kesi ya madai ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa mbunge jimbo la Ilemela.
 
Kesi hiyo imefutwa kutokana na ombi maalumu la mleta shtaka Hynes Kiwia kutaka kupunguziwa gharama za kuendesha kesi hiyo jambo ambalo lilishindikana kutokana na ombi hilo kutokidhi vigezo.

Katika shauri hilo lililofunguliwa mwaka jana Hyness Kiwia aliye mbunge wa jimbo la ilemela kupitia UKAWA aliwashitaki Angelina Sylivester Mabula ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Jimbo hilo kupitia chama cha Mapinduzi CCM.

Shauri hilo limefutwa na msajili wa mahakama kuu kanda ya mwanza Eugenia gerald na kushuhudiwa na mawakili wa pande zote mbili.

No comments:

Post a Comment