Uongozi
wa Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau wa sheria wanatarajia
kutoa elimu ya sheria katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es
salaam.
Hayo
yamesemwa na Mtendaji Mkuu wa Mahakama Hussein Kattanga alipokuwa
akisisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi kupata elimu hiyo.
‘’Natoa
wito kwa wananchi kuhudhuria maadhimisho ya siku ya sheria nchini
yanayoashiria kuanza mwaka mpya wa shughuli za mahakama”Alisema
Kattanga.
Kauli mbiu katika maadhimisho hayo ya mwaka huu ni “huduma za haki kumlenga mwananchi:wajibu wa mahakama na wadau”
Ameongeza
kuwa,miongoni mwa wadau watakaoshiriki katika kutoa elimu ya sheria ni
pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Taasisi ya Sheria kwa
Vitendo Tanzania (Law School), Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS),
Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA),Tume ya Haki za Binadamu na
Utawala Bora,Takukuru pamoja na Polisi.
Aidha Kattanga amesema kwamba wadau hao watatoa huduma za kisheria na kimahakama kwahiyo
wananchi wenye mashauri ya muda mrefu,malalamiko yoyote na mapendekezo
ya uboreshaji wa utendaji kazi wa mahakama wafike na kuonana na
waheshimiwa Majaji, Mahakimu,Wasajili na Watendaji wa Mahakama.
Maadhimisho
hayo hufanyika nchini kila mwaka katika wiki ya kwanza ya mwezi wa pili
ambapo kwa Jiji la Dar es salaam inatarajia kufanyika tarehe 31 Januari
hadi Februari 3.
No comments:
Post a Comment