Mradi wa Mabasi ya mwendo kasi kutarajiwa kuanza kazi Januari 10
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa
akisalimiana na watendaqji mbalimbali wa mradi wa mabasi yaendayo
haraka waliofika katika kituo cha Feri cha Mradi wa Mabasi yaendayo
haraka (BRT) leo jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa akitembelea maeneo mbalimbali ya kituo cha Feri jijini Dar es Salaam leo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Majaliwa akipanda basi la mwendo wa haraka mara baada ya kutembelea
maeneo mbalimbali katika kituo cha feri leo jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa akiwa
katika kituo cha Mradi wa mabasi cha Jangwani kukagua maendeleo ya
ujenzi ya kituo hicho ikiwa ujenzi wa kituo hicho upo hatua za mwisho
kukamilika.
Kituo cha Mradi wa mabasi yaendayo
haraka kikiwa kimekamilika na mabasi yakiwa nyuma ya kituo hiki kwaajili
yakisubiri kumalizika kwa barabara ili ifikapo Januari 10, 2016 kuanza
kufanya kazi.
Mabasi ya mwendo wa haraka yakiwa kwenye maegesho.
Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa Majaliwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam leo mara baada ya kumalizia kukagua ujenzi wa barabara ya mradi
wa mabasi yaendayo haraka katika kituo cha Morocco jijini Dar es Salaam.
MRADI wa Mabasi
yaendayo kasi (BRT) kuanza Januari 10, 2016 hayo yamesemwa na Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa wakati akikagua ujenzi wa miundo mbinu ya
Mradi wa Mabasi yaendayo haraka leo jijini Dar es Salaam.
Pia Majaliwa amewaagiza watendaji wizara ya
Tamisemi ambao ni wamiliki wa mradi huo kusimamia vyema ili uanze
kufanya kazi kama ilivyo pangwa kwa kuwa mabasi 120 yalishawasili
jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu ameanza kwa kukagua vituo vya mradi
huo kuanzia cha Feri, Jangwani, Kimara na kumalizia na Morocco na
kuwapongeza kwa kumaliza kujenga vituo 15 kati ya 27 na amewaagiza
kumalizia vituo vilivyo baki ili kufikia januari 10 mwakani mabasi
yaanze kufanya kazi.
No comments:
Post a Comment