aanzisha kampeni ya “Mpishe mzee kwanza apate huduma”
Aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dkt. Diwani Msemo. |

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiwa kwenye opareshen ya kutumbua majipu, baada ya kumaliza Dar es salaam akitokea Hospitali ya Ocean Road ambako alimtimua kazikaimu mkurugenzi, sasa ameingia mkoani Tanga ambako ameagiza vituo vyote vya serikali vya kutolea huduma za afya nchini, kuweka anuniani inayosema”Mpishe mzee kwanza apate huduma”.
Ametaka maneno hayo kuandikwa kwenye dirisha la mapokezi, vyumba vya madaktari na sehemu ya dawa.
Agizo hilo amesema linakwenda sambamba na uwepo wa madirisha ya wazee katika vituo vyote vya serikali vya kutolea huduma za afya.
Mhe Ummy pia ameahidi kupeleka Bungeni Muswada wa Sheria ya Taifa ya Wazee katika Bunge ili kuhakikisha haki na stahili za wazee nchini zinatekelezwa kikamilifu.
Wazee walieleza kero zao kubwa ni kupata matibabu, kutokuwa na kipato cha uhakika na vitendo vya kudharauliwa na jamii.
Kauli ya Waziri huyo ilitolewa katika mkutano wake alioufanya katika ukumbi wa Mkuu wa mkoa wa Tanga.
Katika mkutano huo ambapo alikutana na wazee wa Tanga wakiwakilisha wenzao wa Tanzania aliuutisha ili kutoa mwelekeo wa vipaumbele vya serikali ya awamu ya tano kwa wazee wa Tanzania.
Vipaumbele hivyo ni pamoja na bima ya afya ili kupata matibabu ya uhakika na kuhakikisha sheria ya Taifa ya Wazee inapitishwa na Bunge ili kuwezesha wazee kufaidi haki na stahili zao ikiwemo kupata pensheni zitakazowawezesha kuendelea na maisha yao bila shaka.
Wazee wa mkoa wa Tanga wakiuliza wakitoa maoni na kumshukuru Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu (hayupo pichani) kwa kuonyesha upendo wa kuwajali katika kuboresha huduma za afya kwa wazee wakati mkutano wake na wazee wa mkoa huo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akipokea risala iliyosomwa kwa niaba ya wazee wa mkoa wa Tanga.
Pichani juu na chini ni baadhi ya wazee wa mkoa wa Tanga waliohudhuria mkutano ulioitishwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu (hayupo pichani).
No comments:
Post a Comment