Mkurugenzi wa Bendi ya Stars, Aneth Kushaba akifuatilia semina hiyo.
GUD newz ikufikie kwako, prodyuza, meneja, msanii ama mdau wa sanaa
kuwa kampuni ya kusimamia haki za muziki Copyright Management East
Africa (CMEA) kwa kushirikiana na COSOTA wameshakubaliana na nchi zaidi
ya tano Afrika zikiwemo Nigeria, Ghana, Afrika Kusini kuwa kazi zozote
za msanii kutoka nchini Tanzania zitakuwa zikilipwa.
Akizungumza katika semina ya ufuatiliaji wa kazi za sanaa na Ugawaji
Mirabaha kwa wasanii iliyofanyika katika Jengo la LAPF, Kijitonyama
jijini Dar, Afisa Mtendaji Mkuu kutoka COSOTA Bi. Doreen Sinare alisema
kuwa tayari wameshafanya makubalino na kuanzia mwakani wasanii wataanza
kulipwa.
“Tutakuwa tunatumia mtindo wa Lock Sheet ambapo sisi kama COSOTA
tutakuwa tunajulishana na nchi nyingine Afrika tulizoingianazo mkataba
endapo zitacheza kazi zetu watakuwa wakitutumia majina ya wasanii hao na
sisi tutakuwa tukiwatumia majina ya wasanii wa kwao ambao kazi zao
zimechezwa redioni.
“Ipo sheria ambayo ilishawekwa kwa TV na redio za ndani ya nchi
kutumia asilimia 60 kuonesha ama kucheza kazi za ndani na asilimia 40
kwa nchi za nje,” alisema Bi. Sinare.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa CMEA, Paul Matthysse ‘P-Funk’ alisema kuwa
wameshafanya majumuisho ya redio na TV Tanzania nzima na kutakuwa na
mchanganuo wa kila nyimbo, bendi, msanii kuangaliwa kazi zake zimechezwa
mara ngapi.
“Tunaamini kwa mfumo huu utamjengea msanii kunufaika kwa kile
anachokifanya. Kutakuwa na code itakayomuwezesha msanii kujua kazi zake
zimechezwa mara ngapi kwa siku,” alisema P-Funk.
No comments:
Post a Comment