TTCL

EQUITY

Tuesday, December 15, 2015

Tumekula msoto sana kwetu - AY

Msanii Ambwene Yesaya alimaarufu kama AY amefunguka na kusema katika maisha yake ilifika wakati kutokana na hali ngumu ya maisha ilipelekea wakati mwingine kula hata pumba.
AY amesema hayo kwenye kipindi cha Mkasi kinachorushwa na East Africa Television, Ay anasema hali hiyo ilisababishwa na ugumu wa maisha baada ya mama yake mzazi kuacha kazi, kutokana na hali hiyo Ay adai ilifanya wakati mwingine washinde njaa jambo ambalo limekuwa katika utamaduni wake mpaka leo anaweza kushinda na njaa na wala asishtuke.

Katika hatua nyingine Ay amesema Mama yake mzazi ambaye kwa sasa ni marehemu ndiye aliyempatia pesa kiasi cha shilingi elfu kumi ili aweze kurekodi kazi yake ya kwanza ambayo kwa kipindi hicho ilikuwa ni shilingi elfu nane kurekodi wimbo mmoja.

Mbali na muziki Ay amesema yeye binafsi si mpenzi wa siasa ila ni mkosoaji katika siasa na anasema kitu kinachofanya asipende siasa ni kitendo cha wanasiasa wetu kutotimiza ahadi zao wanazotoa kwa wananchi, amedai pia kuonyesha hisia kwa upande wa wasanii kuna pande mbili kumuongezea mashabiki msanii husika au kumpunguzia baadhi ya mashabiki ambao hawatapendezwa na upande wa msanii husika katika siasa.

No comments:

Post a Comment