Kufuatia kukithiri kwa vitendo vya ukatili dhidi
ya watoto ikiwemo kupigwa na kunyanyaswa na kunyimwa fursa ya kupata
elimu ,baraza la Watoto wilaya ya Arusha limeiomba serikali ichukue
hatua kali dhidi ya watakao bainika, ili kukomesha vitendo hivyo
Mwenyekiti wa Baraza la watoto la wilaya ya Arusha, Dominic Raphael
Hayo
yameelezwa katika Baraza la watoto la wilaya ya Arusha lilokutana
kujadili masuala mbalimbali ikiwemo haki za watoto ,Mjumbe wa Baraza
hilo Hassan Kimaro amesema kuwa ili kuwa na taifa bora lenye ustawi ni
vyema kukemea vitendo vya kikatili kwa watoto ili visigeuke desturi na
kuathiri maendeleo ya taifa
Mwenyekiti wa Baraza hilo Dominic Raphael na Mjumbe wa Baraza hilo
Brina Salvatory, amesema kuwa kwa sasa wamejikita katika kutetea haki
za hususan wale wanaofichwa majumbani na kuhakikisha kuwa wanafichuliwa
ili waweze kupata haki zao za msingi ikiwemo elimu na mlo bora
Mratibu wa wanawake na watoto jiji la Arusha ,Saumu Kweka amesema
kuwa Baraza hilo la watoto limesaidia kufichua vitendo vya kikatili
dhidi ya watoto na kuziwezesha mamlaka husika kuchukua hatua kali.
Changamoto inayowabili watoto nchini ni pamoja na matukio ya kikatili
wanayofanyiwa majumbani ambayo asilmia kubwa hayaripotiwi katika vyombo
vya sheria ,suala linalofanya ukatili wa kijinsia kukosa mwarobaini wa
kisheria ambao unaweza kukomesha vitendo hivyo.
No comments:
Post a Comment