Mwenyekiti
wa kampuni ya Quality Group, Yusuf Manji amemwandikia barua Rais John
Magufuli kumuelezea mchakato wa zabuni aliyoshinda kuendeleza ufukwe wa
Coco maarufu kama Coco Beach uliopo Kinondoni.
Taarifa
iliyotolewa na kampuni hiyo kwa vyombo vya habari jana ilisema Manji
aliandika barua hiyo Desemba 5 mwaka huu akimuelezea kiongozi huyo wa
nchi usahihi wa mchakato wa zabuni ya kuendeleza eneo hilo akiwa
ameambatisha majibu ya pendekezo la mradi huo kuwa lilitakiwa
kutekelezwa na kampuni tanzu ya QGL, Q Consult Ltd.
Alisema kampuni hiyo ilishinda zabuni kwa kufuata masharti na vigezo vilivyokuwa vimependekezwa na Manispaa ya Kinondoni.
Manji
katika barua hiyo alionekana “kuisemelea” Manispaa hiyo kuwa Januari
20 mwaka huu QCL aliiandika barua yenye kumbukumbu namba QCL/KMC/01/15
ili kusuluhisha kesi hiyo iliyokuwa mahakamani kwa muda mrefu, lakini
Manispaa waliidharau.
Alisema
hakuna kipengele katika pendekezo la QCL kinachohusisha uuzaji wa
ardhi wala kuzuia umma kufika kwenye ufukwe, na badala yake ilitilia
mkazo mandhari nzuri kwa shughuli za kijamii na burudani kwa umma kama
ilivyo katika muongozo uliotolewa na KMC na Sheria ya Usimamizi wa
Mazingira.
“Kwa
dhumuni la kutoonyesha upendeleo, katika barua yangu kwa Mheshimiwa
(Rais Dk Magufuli), niliomba afanye uchunguzi binafsi chini ya ofisi
yake tukufu ambayo nitashirikiana nayo kikamilifu na nitakubaliana na
hukumu ya itakayotokana na taarifa sahihi na za haki,” alisema Manji.
No comments:
Post a Comment