Toleo la 436
Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke, mipango miji, machinga, kero vijijini na waishiwa, Uzitoni Street, Bongo.
Duh, hatimaye mpenzi!
Hatimaye! Hata kama umechelewa kuonekana kama Waziri wa Elimu wa mheshimiwa wetu, hatimaye umekuja. Bado ni kama naeleaelea angani kwa furaha niliyo nayo. Bado nakushukuru kwa kuniaminisha kwamba mi bado wako nawe bado wangu! Bado, niko tayari kuvumilia hadi tukamilishe mipango yetu pamoja ili tuwe pamoja daima. Asante mpenzi, asante. Linalobaki sasa ni kutofukuzwa kazi na Mama Bosi eti nazidi kuimba kazini.
Mabosi Bwana! Nikisononeka anaona nimechoka kazi hivyo bora niondoke. Nikiimba kwa furaha, lazima nimeiba mahali ndiyo maana nafurahi hivyo. Kaazi kwelikweli. Mbona hata mumewe kaimba siku nzima baada ya kuteuliwa tena kuwa Waziri katika Baraza la Mheshimiwa wetu H2K.
‘Unaona mke wangu? Unaona faida ya kuwa uaminifu? Hivi vikinda vya jana vinahitaji busara za sisi wazee pia. Lazima tufanye sherehe.’
MB akatingisha kichwa.
‘Mume wangu, huoni enzi za sherehe zimekwisha. Hapa kazi tu, si wiski.’
‘Kwani tukifanya hapa nyumbani kuna ubaya gani?’
‘Na utawaalika akina nani? Lazima wako wapambe ambao wanajikweza kwa kuwakwaza wengine.’
Bosi akainamisha kichwa.
‘Ni kweli mke wangu. Mara nyingine najiuliza kuna faida gani kuwa Waziri.’
Wakati huo huo, Binti Bosi aliingia na kusikia maneno yake.
‘Ahaa! Unaona sasa. Miaka na miaka unaniimbia kuhusu unavyojitoa kutumikia taifa, niache kukosoa wakati mnashinda na kukesha kwa nia ya kuwatumikia wananchi. Kumbe …’
‘Usinisumbue. Siwezi kutania?’
BB hakusema neno lakini alinyanyua kope lililozungumza kwa niaba yake.
‘Sawa baba.’
‘Sawa ndiyo. Halafu hujaona jina la Wizara sasa?’
BB akacheka.
‘Nimeona mheshimiwa Waziri wa Mikiki na Makeke, mipango miji, machinga, kero vijijini na waishiwa’
‘Usicheke. Huoni kwamba ni kazi ngumu?’
‘Hapana Baba. Mbona naona vyote vinahusiana na mikiki na makeke. Mipango Miji, mikiki. Machinga, kero vijijini na waishiwa makeke. Ni mwendelezo wa kazi yako tu. Hebu angalia ya kwetu.’
‘Ya kwenu ipi?’
‘Ya vijana. Mimi nilifikiri safari hii tutakumbukwa na kujaliwa. Lakini hebu ona sasa, sisi tuko ndani ya Wizara gani.’
Bosi akacheka.
‘Tuone kama utaweza hata kuitamka.’
‘Tumeshabatiza baba. Ni Wizara ya SEBUKAVIAWA.’
MK akashangaa.
‘`Huyu ni mnyama gani jamani?’
‘Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu.’
‘Duh!’
Bosi akasema.
‘Lakini angalau mna manaibu wawili.’
‘Haisaidii baba. Mbele ya Sera na Bunge, na ajira, vijana tunaona ndani kweli? Tutabaki kaidara kasikoonekana kama kawaida yake. Aaaagh!’
‘Lakini mbona wewe unang’ang’ania sana vijana. Mnastahili kweli kutiliwa maanani kuliko Bunge?’
‘Kwa nini tusitiliwe maanani. Sisi ni taifa la leo, sisi ni walio wengi, na mustakabali wa taifa unatutegemea sisi. Lakini kila mara tunawekwa ndani ya wizara yenye jina refu na bajeti fupi. Na mbele ya marupurupu yenu, inawezekana vijana wasipata hata senti tano.’
‘Na walemavu je?’
‘Na walemavu pia. Bora kutotutaja kabisa kuliko kuturundika sote chini na mwamvuli mmoja. Mvua ikinyesha, tutakaolowa na vijana na walemavu nakuambia.’
Bosi akazidi kucheka kwa kejeli.
‘Shauri zenu vijana.’
BB akaonyesha kukasirika.
‘Shauri zenu pia. Nilifikiri uchaguzi uliopita uliwapa somo kidogo. Ndiyo mlishinda lakini vijana waliwatingisha. Umoja wenu feki haukuonekana mahali popote kwa sababu haujawahi kutetea vijana hata mara moja.Lakini bado unawadharau. Nilipinga na rafiki yangu shuleni kwamba hatuwezi kuwekwa kwenye wizara yenye jina refu kuliko ila ya awamu iliyopita, sasa imekuwa refu zaidi mara mbili. Duh!’
‘Nyinyi vijana hamtutishi. Hii ni nchi ya wazee. Wazee ndio wenye busara …’
Bosi alionekana anataka kutoa hotuba lakini alikuta BB anamwimbisha kama vile yuko kwenye kwaya.
‘Unaona. Hata wewe unakosa heshima kwa wazee kisha mnadai kuheshimiwa.’
‘Hapana baba. Wazee wanadai kuheshimiwa huku vitendo vyao si vya heshima hata kidogo. Kila siku eti vijana wa siku hizi … vijana wa siku hizi … mbona hatuongelei wazee wa siku hizi. Walevi, mafisadi …’
Na BB alionekana kutaka kutoa hotuba lakini akakuta baba yake anamwimbisha na yeye. Ikabidi acheke.
‘Haya Baba mechi droo, iwapo refa ni refa kweli.’
‘Una maana gani?’
‘Mmeweka mpenzi wa goli ya mkono kuwa waziri wa michezo, kisha anasema ataleta nidhamu? Atahalalisha magoli ya mkono au?’
‘Ohoo umeanza mambo zako.’
‘Kwani uongo baba. Labda tutunge sheria mpya mchezoni. Kabla ya mchezo, ijulikane refa yuko upande gani. Kisha upande wake yanaruhusiwa magoli ya mkono matatu. Upande mwingine, hata wakifunga kwa mguu, magoli matatu yatakataliwa kwa kuwa walifanya faulo isiyoeleweka. Na iwapo hawa bado wanaelekea kushinda mechi itasimamishwa kwa utovu wa nidhamu ili irudiwe tena baadaye.’
Bosi akamwangalia mwanaye.
‘Yaani wewe unajitia mjanja sana siyo.’
‘Hapana baba. Lakini alisema hakusema?’
‘Alisema.’
‘Na sasa anataka kuleta nidhamu hataki?’
‘Anataka.’
BB akacheka.
‘Basi mheshimiwa baba naomba kuwakilisha.’
Nilifikiri bosi atapasuka kwa hasira lakini baada ya kumwangalia mwanaye, akapasuka kwa kicheko.’
‘Wewe kweli sikuwezi. Ndiyo maana tunaficha vijana ndani ya mambo yooooote yale mengine. Hata tukijaribu kuwafunika, mnazidi kufurukuta. Nina wasiwasi mtafunika hata bunge katika wizara hii.’
‘Sasa hebu fikiria tungefanya mangapi tungepewa nafasi ya kweli. Hata mipango yote ya bosi wako yangefanikiwa haraka sana.’
Bosi akacheka tena na hakutaka kusema zaidi. Lakini kweli mpenzi wangu wa moyo, kwelikweli, unaweka vijana ndani ya wizara yenye majukumu makubwa kibao, na hata waheshimiwa ambao kwa midomo yao watasikilizwa tu. Kila siku wanadai eti vijana hatuna uzalendo. Wao wana uzalendo kwetu?
Na njoo tena na tena mpenzi, mke wako mtarajiwa azidi kupaa angani
Akupendaye usiku na mchana, kwa urefu na upana, kwa kazi na mabadiliko
Hidaya

No comments:
Post a Comment