Eneo la ndani la uwanja wa ndege wa KIA.
KAMPUNI
ya maendeleo ya viwanja vya ndege (KADCO) inayosimamia uwanja wa ndege
wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) imekoa zaidi ya kiasi cha sh Bil 2
katika kipindi cha wiki moja ikiwa ni thamani ya nyara za serikali na
vito vya thamani vilivyokuwa vitoroshwe kupitia uwanja huo.
Menejimenti
ya uwanja huo kupitia kitengo cha usalama kiwanjani hapo ilifanikiwa
kukamata kunasa vipande 264 vya madini ya Tanzanite vikiwa na uzito wa
kilograamu 2.04 ambavyo thamani yake inakadiriwa kufikia Bilioni 2.5.
Vingine
vilivyokamatwa uwanjani hapo vikiwa njiani kusafirishwa kuelekeaa
nchini Vietnam ni pamoja na kucha 261 ,meno 60 ya Simba ambayo yanadaiwa
kutokana na kuuawa kwa Simba 13 .
Kaimu
mkurugenzi wa KADCO,Bakari Murusuri aliiambia Globu ya jamii kuwa
Desemba 18 ,maofisa usalama uwanjani hapo walimkamata abiria mwenye
asili ya Uarabuni akiwa na pembe mbili za Twiga.
“Siku
ya Ijumaa tulimkamata abiria mwingine mwenye asili ya kiarabu,akitaka
kutorosha pembe mbili za Twiga na baada ya tukio hilo Jumamosi katika
ndege ya Ethiopian airlines walikamatwa abiria wengine raia wa kigeni
wakitaka kutorosha Pembe mbili za Impala nao walishikiliwa na
kukabidhiwa kituo cha polisi cha KIA.”alisema Murusuri.
Aliyekamatwa
akiwa na Pembe za Tiwiga ametajwa na idara ya uhamiaji kuwa ni Jasim
Mbarakke Alh-kubaisi (43) ambaye anaidaiwa kuwa ni mlinzi wa mfalme wa
nchi ya Qatar iliyopo katika falme za kiarabu.
“Ukiangalia
haya matukio ndani ya wiki moja ,tumeweza kuokoa kiasicha fedha
zisizopungua Bilioni mbili za kitanzania,kama viongozi wengine katika
viwanja vingine ,mipakani a taasisi nyingine ila mmoja atashuhudia
serikkali yetu inavyoweza kujiondesha kwa kodi za ndani”aliongeza
Murusuri.
Alisema
katika uwanja huo kumekuwa na matukio mengi ambayo hayakuripotiwa
kwenye vyombo vya habari yakiwemo ya kukamatwa kwa watu 11 wakisafirisha
dawa za kulevya katika kipndi cha miaka miwli iliyopita.
“Matukio
yamekuwa yakitokea mengi ,ndani ya miaka miwili iliyopita katika uwanja
huu tumekamata watu wasio pungua 11 wakijaribu kupitisha dawa za
kulevya na tayari wamefikishwa mbele ya vyombo vya sheria ikiwemo
wengine kufungwa jela.”alisema Mrusuri.
Murusuri
alisema kwa sasa katika uwanja huo kumefungwa vifaa vya kisasa ambavyo
vinahakikisha kwa hakuna mtu anaye pita uwanjani hapo na vitu ambavyo
havijaruhusiwa kisheria ikiwa ni jitihada za kumuunga mkono rais wa
Jamhuri ya muungano wa Tanzania ,John Magufuli.

Mapema wiki iliyopita jeshi la Polisi mkoani
Kilimanjaro lilitoa taarifa ya kushkiliwa kwa watu wanne wakiwamo raia
wanne kutoka mataifa tofauti kwa makosa mbalimbali, akiwemo aliyekutwa
na nyara za serikali kinyume cha sheria.Kamanda wa polisi mkoani hapa, Fulgence Ngonyani alisema tukio la kwanza lilitokea Dec 15 majira ya saa 10.00 alasiri katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), ambapo alikamatwa raia wa Vietnam,Hoang Nghia Trung(49) akitaka kusafirisha nyara hizo.Alisema mtuhumiwa huyo alihifadhi nyara hizo katika mabegi yake ambapo maofisa
wa usalama katika uwanja wa ndege wa KIA walimtilia shaka na kufanya
upekuzi katika mabegi yake ndipo walipokuta nyara hizo zikiwa
zimehifadhiwa ndani ya mabegi hayo.
Hata
hivyo thamani halisi ya nyara hizo bado haijajulikana na mtuhumiwa
anaendelea kuhojiwa na atafikisha mahakamani mara upeleleziutakapokamilika.
Katika tukio jingine ,Anurag Jain(45) raia wa India alikamatwa uwanja wa ndege wa Kia akiwa na madini ghafi aina ya Tanzanite vipande 264 bila kibali akiwa amehifadhi kwenye mabegi yake akielelekea Hong Kong C
|
No comments:
Post a Comment