Urembo na Mapambo
- Bangili, hereni na mikufu unayoitumia mara kwa mara vinafaa vitundikwe kwenye stand maalumu mahali panapofikika kiurahisi mfano juu ya dressing table ili iwe rahisi kuvichukua na kutumia kila unapohitaji na kuzuia visishikane na hatimaye kuharibika.
- Vito vya thamani viwekwe mahali salama kwenye container au box dogo zikizungushiwa kitambaa laini au sponji ili kuhifadhi thamani na mng’ao wake.
- Hifadhi vitu vya aina moja pamoja, mfano dhahabu, silva, plastic, shanga, n.k ili iwe rahisi kujua kitu fulani kipo wapi kinapojitajika.
- Hakikisha mikufu yote imefungwa vyema kuepuka kushikana na hatimaye kukatika.
Pochi na Mpangilio Wake
Pochi ni kitu ambacho wanawake tumezoea sana kukitumia na huwa zinatufaa sana katika mizunguko yetu mbali mbali iwe kazini, kanisani, klinik au hata sokoni.
Wengi wetu utakuta tuna pochi zaidi ya moja na mara nyingi utakuta mtu anabadilisha pochi kwa wiki labda mara moja au mbili. Tatizo linakuja pale ambapo unakuta mtu unabadilisha pochi asubuhi na ukifika kazini unakuta umesahau simu, ufunguo au hata pesa kwenye pochi ambayo ulitumia jana.
Ili kuepuka tatizo hili kuna vipochi vidogo (siyo wallet) kama hicho hapo kwenye picha ambacho unaweza kuweka vitu vyote vidogo vidogo kama diary, simu, wallet, miwani, kalamu, lipstic, perfume n.k katika mpangilio maalum na ukitaka kubadili pochi unakichukua hiki kipochi chote na kuamishia kwenye pochi kubwa.
Pia hii itakusaidia kutoa vitu kwa urahisi ndani ya pochi maana mara nyingine simu inaweza ikaita hadi ikakatika bila wewe kuipata maana pochi ni kubwa na ina vitu vidogo vidogo vingi vyote vimerushiwa tu. Mara zote hakikisha pochi yako imepangwa vizuri na haijajazwa sana hadi kuharibu uzuri wake na uhalisia wake.

- kama viatu pochi pia zinapendeza na pia kukusaidia kuokoa muda zikihifadhiwa kwa ukubwa, rangi, aina au matumizi.
- Pochi unazotumia mara kwa mara weka kwenye stand maalumu na nyingine unaweza weka kabatini ili kupunguza wingi wa vitu kutundikwa kila mahali.
- Pochi ndogo na wallet ziwekwe pamoja ndani ya droo au pochi kubwa ili kuepuka kupotelea ndani ya nguo au pochi nyingine.
Namna ya kupangilia Nguo
Mara nyingi unaweza kukuta mtu ana kabati limejaa nguo hadi zinakosekana pa kuwekwea na katika hali halisi anajiona hana nguo za kuvaa. Hali hii inatokana na kukosa mpangilio wa nguo kwenye kabati na pia kuweka nguo ambazo hazihitajiki tena. Nguo zisipokuwa na mpangilio maalumu ni ngumu sana kutafuta nguo gani uivae na ipi maana hujui ipo upande gani wa kabati. Pia pale unapohifadhi nguo ambazo unajua hutazivaa tena inasababisha kabati kujaa bila sababu. Njia hizi zitakusaidia katika kupanga kabati lako:
1. Tafuta siku ambayo unamuda wa kutosha na toa nguo zako zote
kabatini kisha tenga zile ambazo unahitaji kuzivaa na zile ambazo unaona
hutazivaa tena ( iwe zimekubana, zimechakaa, hauzitaki tena n.k).
2. Tafuta mfuko safi uweke nguo zote ambazo hutazivaa tena ambazo upo tayari kugawa kwa wenye uhitaji. Ni vyema ukianzia nyumbani mwako, kama una dada wa kazi unaweza mpa zile ambazo zitamfaa na kisha nyingine ukapelekea wengine wenye mahitaji unaowafahamu kama ni kanisani au mahali popote pale. Ila jihadhari usimpe mtu nguo iliyochakaa sana, haipendezi.
3. Nguo ambazo unazihitaji zitenge katika makundi (blauzi, sketi, magauni, n.k) na kisha uzikunje vizuri na kuzipanga kabatini kila kundi sehemu yake. Hii itakusaidia ukiwa unatafuta gauni unajua uangalie sehemu gani. Nguo zinazoendana pamoja kama suti au vitenge ni vyema zikawekwa pamoja sketi na blauzi yake. Kama kabati lina nafasi kubwa makoti ya suti yakiwekwa kwenye henga yanapendeza zaidi.
4. Vitu kama mikanda, skafu, mitandio n.k viwekwe mahali pake ili iwe rahisi kupatikana pale vinapohitajika.
Jitahidi uwe na tabia ya kupanga nguo zako kila unapozifua. Ilikuepuka kutafuta nguo asubuhi na hatimaye kuharibu mpangilio wa kabati lako ni vyema kama utakuwa na utaratibu wa kunyoosha nguo za wiki zima kila mwisho wa wiki, hii itaokoa muda na ‘stress’ za kutafuta nguo ya kuvaa kila asubuhi.
Mara nyingi unaweza kukuta mtu ana kabati limejaa nguo hadi zinakosekana pa kuwekwea na katika hali halisi anajiona hana nguo za kuvaa. Hali hii inatokana na kukosa mpangilio wa nguo kwenye kabati na pia kuweka nguo ambazo hazihitajiki tena. Nguo zisipokuwa na mpangilio maalumu ni ngumu sana kutafuta nguo gani uivae na ipi maana hujui ipo upande gani wa kabati. Pia pale unapohifadhi nguo ambazo unajua hutazivaa tena inasababisha kabati kujaa bila sababu. Njia hizi zitakusaidia katika kupanga kabati lako:

2. Tafuta mfuko safi uweke nguo zote ambazo hutazivaa tena ambazo upo tayari kugawa kwa wenye uhitaji. Ni vyema ukianzia nyumbani mwako, kama una dada wa kazi unaweza mpa zile ambazo zitamfaa na kisha nyingine ukapelekea wengine wenye mahitaji unaowafahamu kama ni kanisani au mahali popote pale. Ila jihadhari usimpe mtu nguo iliyochakaa sana, haipendezi.
3. Nguo ambazo unazihitaji zitenge katika makundi (blauzi, sketi, magauni, n.k) na kisha uzikunje vizuri na kuzipanga kabatini kila kundi sehemu yake. Hii itakusaidia ukiwa unatafuta gauni unajua uangalie sehemu gani. Nguo zinazoendana pamoja kama suti au vitenge ni vyema zikawekwa pamoja sketi na blauzi yake. Kama kabati lina nafasi kubwa makoti ya suti yakiwekwa kwenye henga yanapendeza zaidi.
4. Vitu kama mikanda, skafu, mitandio n.k viwekwe mahali pake ili iwe rahisi kupatikana pale vinapohitajika.
Jitahidi uwe na tabia ya kupanga nguo zako kila unapozifua. Ilikuepuka kutafuta nguo asubuhi na hatimaye kuharibu mpangilio wa kabati lako ni vyema kama utakuwa na utaratibu wa kunyoosha nguo za wiki zima kila mwisho wa wiki, hii itaokoa muda na ‘stress’ za kutafuta nguo ya kuvaa kila asubuhi.
Viatu na Matumizi Mbalimbali

Viatu ni kinga kwa ajili ya kuhifadhi miguu. Vile vile viatu ni vazi ambalo linaongeza urembo na nakshi kwa mvaaji. Viatu vipo vya aina mbalimbali na vinavaliwa kulingana na mahali na mavazi yanayoambatana navyo. Tuangalie baadhi ya aina za viatu na wapi hasa na vipi vikitumika vinapendeza zaidi.
1.Viatu vya ngozi vya kufunika
Viatu vya kufunika vipo virefu sana, vyenye urefu wa wastani na vifupi kabisa. Mara nyingine haviwi vya ngozi kabisa bali ni kama vina plastiki na pia vingine huwa na uwazi mdogo kwa mbele.Viatu virefu zaidi mara hupendeza zaidi kuvaliwa kwenye sherehe na kanisani. Unaweza kuvaa kazini kama kazi yako haikulazimu kutembea tembea maana vitachosha miguu yako na kupunguza ufanisi.
Viatu vyenye urefu wa wastani unaweza kuvaa popote iwe kazini, kanisani, kwenye sherehe n.k. Viatu vya chini kabisa vinakuwa vyenye matumizi zaidi wakati unamatembezi mengi. Havifai sana kuvaa kwenye sherehe za usiku hasa kama unavaa nguo maalumu ya usiku. Vinafaa sana kwa mjamzito hasa katika miezi ya mwisho.
2.Viatu vya wazi virefu
Viatu hivi vipo vya aina mbili, vyenye rangi za mng’ao na ambavyo ni mahususi kwa sherehe za usiku na vyenye rangi ngumu ambavyo waweza kuvaa kazini au kanisani. Viatu hivi vinapendeza kuvaliwa na nguo yoyote ila ikiwa ya urefu wa wastani ni nzuri zaidi maana huwezesha kuonekana urembo na uzuri wote wa kiatu. Viatu hivi vinakuja katika mitindo mbalimbali na unachagua ule ambao wewe unaupendelea zaidi mfano vyenye visigino vyembamba, visigino vinene au aina ya ‘wedges’.
3.Viatu vya wazi vifupi
Viatu hivi ni vizuri sababu vinawezesha miguu kupumua na ku’relax’. Viatu hivi vipo vya aina tofauti tofauti na vinafaa sana kuvaliwa kwa matembezi ya jioni, wakati wa safari ndefu, wakati ukiwa na mizunguko mingi na pia hata kazini au kanisani pale unapokuwa umevaa nguo za kawaida (casual). Havivutii sana kuvaliwa na suti au nguo ya usiku. Pia mara nyingi viatu vya chini hupendezea kuvaliwa na nguo ndefu( hasa casual) na viatu virefu hupendeza zaidi kwa nguo yenye urefu wa wastani.
4.Viatu vya muda maalumu
Hivi ni viatu ambavyo vinavaliwa wakati wa kazi maalumu kama wakati wa kazi za mashambani, mgodini, wakati wa michezo au wakati wa baridi kali.
Ni vyema na inapendeza kama unauwezo uwe na viatu vya aina mbalimbali angalau aina tatu. Mfano viatu vyeusi vya urefu wa wastani, viatu vya usiku vya wazi, viatu vya chini vya kufunika na vya wazi.
Namna ya kuhifadhi kwa mpangilio Viatu
- Viatu unavyovivaa mara kwa mara viweke kwenye ‘shoe rack’ mahali ambapo ni rahisi kuonekana kama ni kwenye korido au sehemu yoyote rahisi kufikika.
- Vipange viatu vyako kwenye shoe rack kufuatana na rangi, urefu wa kisigino, aina ya kiatu au matumizi.
- Hakikisha viatu vyako ni vikavu na safi kabla ya kivihifadhi na hifadhi sehemu kavu isiyo na maji au unyevu.
- Viatu ambavyo havivaliwi mara kwa mara kama vile vya kuvaa kwenye matukio maalinu ya usiku ni vyema vikihifadhiwa kwenye sehemu ya chini ya kabati.
No comments:
Post a Comment