TTCL

EQUITY

Saturday, December 12, 2015

Harmonise aguswa na kasi ya Magufuli

Harmonise, msanii wa muziki ambaye ameibuka kwa kasi katika chati za muziki wa Bongo Fleva, akiwakilisha kundi kubwa la mashabiki wake, amekuwa ni moja kati ya wasanii ambao wamezungumza juu ya kuridhishwa na kasi ya utendaji wa Rais Magufuli.

Harmonise
Rais Dkt. Maguful
Kama utaratibu wetu eNewz ulivyo, kupima joto la kisiasa katika kila kinachoendelea kutoka kwa wasanii na wadau wa burudani, kwa upande wa Harmonise amesema Magufuli anaonesha mwanga na matumaini ambayo yalikuwa yamepotea kwa watanzania wengi, akihusisha suala zima la kusherehekea uhuru kwa kufanya kazi ya usafi, kuundwa kwa baraza dogo la mawaziri kati ya mambo mengine, kitu ambacho ni cha kushukuru Mungu.



Ikiwa leo pia baraza jipya la mawaziri lililotangazwa na Rais Magufuli limeapishwa, kama sehemu ya wanajamii, msanii huyo anayetikisa chati na ngoma ya Aiyola, anaungana na mastaa wengine wengi wa Tanzania, wengine wakichukua hatua ya kutengeneza wimbo kutoa maoni yao mbalimbali kuhusiana na uongozi mpya hapa Tanzania.

No comments:

Post a Comment