Chama cha Wananchi CUF kimesitisha ajenda yao ya
kurejesha kwa wananchi mpango wa kupinga uamuzi wa Mwenyekiti wa Tume ya
Uchaguzi Zanzibar ZEC, kufuta matokeo ya uchaguzi baada ya juhudi za
kidiplomasia kuonyesha muelekeo wa kupata ufumbuzi.
Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF, Maalim Seif Sharif Hamad. |
Akiongeza
na Waandishi wa Habari jana Katibu Mkuu wa Chama hicho ambaye pia ndiye
Mgombea Urais wa chama hicho Visiwani Zanzibar Maalim Seif Sharrif
Hamad amesema juhudi sasa zimeanza kuonekana katika kulitafutia ufumbuzi
suala hilo.
Maalim Seif amesema Juhudi zinazochukuliwa na Jumuiya ya Kimataifa katika kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huo ikiwemo umoja wa Mataifa zinaonyesha muelekeo mzuri na kuwataka wananchi kuwa watulivu wakati huu.
Hata hivyo Maalim Seif amesema kuwa kuna kikundi cha Watu wachache ambacho kimekua kikwazo kutokana na kutetea maslahi binafsi katika kutafuta muafaka wa mgogoro huo.

No comments:
Post a Comment