KWANZA kabisa tumshukuru Mungu kwa kutuweka hai, hakika yeye anastahili kuabudiwa kila siku.
Baada ya kusema hayo nianze kwa kuwataka wasomaji wangu kutafakari kwa kina hizi ajali za mabasi zinazotokea mara kwa mara katika barabara za nchi yetu.
Kwa muda wa siku zisizopungua kumi na nane zimetokea ajali mbaya za mabasi na kusababisha Watanzania wenzetu zaidi ya ishirini na kenda kupoteza maisha. Kule Mkata, Handeni Tanga watu kumi walifariki dunia baada ya mabasi kugongana na njia ya Mikumi, Morogoro mabasi yaligongana na watu wawili waliaga dunia na kuacha wengi wakiwa majeruhi.
Jumapili iliyopita katika eneo la Ruaha Mbuyuni basi liligongana na Fuso na kusababisha watu kadhaa kufariki dunia na wengine kujeruhiwa baada ya magari hayo kuwaka moto mara baada ya kugongana.
mfululizo wa ajali zinazoendeleakutokea katika maeneo mbalimbali ya nchini Tanzania juma hili, ikiwa ni siku moja baada ya watu watano kufariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mikoa ya Dodoma na Iringa, jana kulitokea ajali nyingine ya Basi la Princes Munaa lililokuwa likitokea Jijini Dar es Salaam kwenda Mwanza, katika kijiji cha Mtanana Kibaigwa Wilaya ya Kongwa Mkoa wa Dodoma. hakuna aliepoteza maisha katika ajali hiyo. zaidi kumetokea majeruhia mabapo, watu kadhaa wamejeruhiwa. Tanzania imekuwa ikishuhudia ajali za mara kwa mara za barabarani ambapo makumi ya watu wamekuwa wakipoteza maisha yao. Uzembe wa madereva na mwendo kasi zinatajwa kuwa sababu kuu zinazosababisha mlolongo wa ajali nchini Tanzania.
Hili ninalolisema polisi ni mashahidi kwa sababu baadhi yao wamewahi kuwakamata madereva wa mabasi wakiwa wamelewa na kuwakataza kusafirisha abiria.Zoezi hilo linatakiwa kuwa la kudumu, kwa sababu tunajua wazi kwamba sasa hivi hakuna utaratibu wa vinywaji vikali kuuzwa na kununuliwa kwenye baa, viroba vinauzwa kila mahali, stendi za mabasi ya kwenda mikoani na hata zile stendi za daladala, Bajaj na bodaboda.
Sasa tuseme basi na kuepuka ajali za kizembe, inawezekana. Wakuwalaumu katika ajali hizi ni madereva wetu wanaopewa dhamana ya kusafirisha abiria. Nasema kuna kitu, bila kumung’unya maneno niseme ukweli tu kwamba baadhi ya madereva ni walevi.
Gari la Princes Munaa lenye namba za usajili T183 CRW likiwa limepiga mweleka.
KWANZA kabisa tumshukuru Mungu kwa kutuweka hai, hakika yeye anastahili kuabudiwa kila siku.
Baada ya kusema hayo nianze kwa kuwataka wasomaji wangu kutafakari kwa kina hizi ajali za mabasi zinazotokea mara kwa mara katika barabara za nchi yetu.

Jumapili iliyopita katika eneo la Ruaha Mbuyuni basi liligongana na Fuso na kusababisha watu kadhaa kufariki dunia na wengine kujeruhiwa baada ya magari hayo kuwaka moto mara baada ya kugongana.
mfululizo wa ajali zinazoendeleakutokea katika maeneo mbalimbali ya nchini Tanzania juma hili, ikiwa ni siku moja baada ya watu watano kufariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mikoa ya Dodoma na Iringa, jana kulitokea ajali nyingine ya Basi la Princes Munaa lililokuwa likitokea Jijini Dar es Salaam kwenda Mwanza, katika kijiji cha Mtanana Kibaigwa Wilaya ya Kongwa Mkoa wa Dodoma. hakuna aliepoteza maisha katika ajali hiyo. zaidi kumetokea majeruhia mabapo, watu kadhaa wamejeruhiwa. Tanzania imekuwa ikishuhudia ajali za mara kwa mara za barabarani ambapo makumi ya watu wamekuwa wakipoteza maisha yao. Uzembe wa madereva na mwendo kasi zinatajwa kuwa sababu kuu zinazosababisha mlolongo wa ajali nchini Tanzania.
Hili ninalolisema polisi ni mashahidi kwa sababu baadhi yao wamewahi kuwakamata madereva wa mabasi wakiwa wamelewa na kuwakataza kusafirisha abiria.Zoezi hilo linatakiwa kuwa la kudumu, kwa sababu tunajua wazi kwamba sasa hivi hakuna utaratibu wa vinywaji vikali kuuzwa na kununuliwa kwenye baa, viroba vinauzwa kila mahali, stendi za mabasi ya kwenda mikoani na hata zile stendi za daladala, Bajaj na bodaboda.
Sasa tuseme basi na kuepuka ajali za kizembe, inawezekana. Wakuwalaumu katika ajali hizi ni madereva wetu wanaopewa dhamana ya kusafirisha abiria. Nasema kuna kitu, bila kumung’unya maneno niseme ukweli tu kwamba baadhi ya madereva ni walevi.
Gari la Princes Munaa lenye namba za usajili T183 CRW likiwa limepiga mweleka.
Ukweli ni kwamba madereva wa vyombo vya moto baadhi yao wanafanyakazi wakiwa wamelewa.
Ipo haja kwa jeshi la polisi kupitia kikosi chake cha usalama barabarani kuliangalia hili kwa sababu ni wazi kwamba watu wengi wanafariki dunia na wengine kupata vilema vya maisha kutokana na uzembe wa mtu mmoja tu, dereva.
Ipo haja ya kuhakikisha madereva wote wanapimwa ulevi, siyo mwanzo wa safari tu bali hata kwenye vituo vingine njiani kwa sababu baadhi ya madereva hufungasha viroba kwenye mabegi yao na kunywa njiani, hivyo kuhatarisha usalama wa abiria na mali zao.
Lakini pia kuna baadhi ya madereva wa mabasi na malori ambao hawazingatii sheria za usalama barabarani kwa ‘kuovateki’ magari kwenye kona au mlimani, hawa nao ni wazembe na uzembe wao husababisha maafa.
Madereva wote wa aina hii wanapogundulika ni vema serikali ikawafungia kuendesha vyombo vya moto badala ya kuwatoza faini kwa sababu makosa wanayoyafanya ni kisababishi cha vifo kwa watu wasio na hatia.
Nimuombe Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Barabarani Tanzania, DCP Mohamed Mpinga kuwa mkali kwa askari wanaowaachia madereva walevi na wanaokiuka sheria za usalama barabarani.Sipendi kumfundisha kazi lakini ipo haja sasa kuhakikisha yeye mwenyewe na maofisa wa ngazi za juu wa kikosi chake wanafanya ukaguzi wa kushitukiza ili kukomesha uzembe huo.
Yeyote anayezembea katika hili achukuliwe hatua stahiki kwa sababu ambazo nimezitoa hapo juu, hakika tumechoshwa kushuhudia wananchi wasio na hatia wakifariki dunia kwa uzembe wa wachache.

No comments:
Post a Comment