Serikali imewasilisha bungeni muswada wa sheria ya udhibiti wa ajira za wageni wa mwaka 2014 huku kubwa likiwa ni kudhibiti utoaji ajira holela kwa wageni hasa zile ambazo zinaweza kufanywa na wazawa.
Waziri wa kazi na ajira Gaudensia Kabaka amesema kupitia muswada huo serikali itaweza kusimamia vyema ajira kwa wageni na kufanya ajira hizo ziwe na tija kwa taifa kuliko ilivyo hivi sasa.
Nayo kamati ya kudumu ya bunge ya maendeleo ya jamii kupitia kaimu mwenyekiti wake Albalt Ntabaliba pamoja na kambi ya upinzani bungeni kupitia msemaji wake katika wizara ya kazi na ajira Cesilia Paresso wamesema ni vyema muswada huo ukaangaliwa kwa makini ili kutatua changamoto zilizopo hivi sasa.
Nao baadhi ya wabunge waliochangia muswada huo wamesema ipo haja ya kuangaliwa kwa dosari zilizopo katika muswada huo na kisha zikarekebishwa sambamba na kuwaandaa wazawa kuajiriwa katika sekta ambazo zinashikiliwa na wageni
No comments:
Post a Comment