TTCL

EQUITY

Wednesday, March 4, 2015

MAJAMBAZI WAUA AFISA MTENDAJI


Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Mpona kata ya Totowe Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya, Bahati Mwanguku (38) ameuawa na majambazi wawili wenye mapanga kisha kuporwa pikipiki na simu ya kiganjani.

Ofisa huyo alivamiwa nyumbani kwake Machi 3, mwaka huu alfajiri ambapo awali majambazi hao walidanganya kuwa walifika kuomba msaada, kwani ng’ombe wao walikuwa wameporwa katika eneo lake.

Vijana wawili, Juhudi Mwanda (19) na Huruma Simfukwe (34) waliolala katika nyumba ya pili, walidai kuwa majambazi hao walibisha hodi na baada ya kutopata jibu lolote, walisisitiza wafunguliwe. Walishauriwa warudi kutakapokucha, lakini majambazi hao waliendelea kusisitiza wafunguliwe mlango.

Baadaye Mtendaji aliwataka waende kwa mgambo anayeitwa Tatizo ili waende eneo la tukio, lakini walikataa, wakidai mgambo huyo ndiye aliyewaamuru waje kwake.

Baada ya mabishano ya dakika 15, majambazi hao walimkamata Huruma Simfukwe na kumfunika kwa shuka usoni, kisha kufungua mlango wa nyumba aliyokuwa amelala mtendaji na kumfunika kwenye uvungu wa kochi, lililokuwa sebuleni na kuanza kumcharanga Bahati Mwanguku kwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake na kupoteza maisha papo hapo.

No comments:

Post a Comment