Kumekuwa na tetesi kuwa waigizaji, JB, Mzee Majuto na Zembwela hivi sasa wapo kazini kutengeneza filamu lakini hadi sasa hawajaamua kuweka wazi swala hili.
Kwamujibu wa watu wa karibu na wasanii hao, inasemekana bado hawajaanza kushuti ila wapo kwenye hatua za awali za maandalizi ya kuanza kufanya kazi , wadau wengi wameonyesha shauku kubwa na kutegemea kazi bora zaidi kutoka kwa wakali hawa kwani itakuwa ni kali ya mwaka.
Kama wewe ni mfuatiliaje wa mitandao ya kijamii utakubali kuwa wakali hawa kwa siku za hivi karibuni wameonekana muda mwingi wakiwa pamoja.
JB kupitia mtandaoni aliweka picha hiyo hapo juu wakiwa pamoja wake kaaa na kuandika kuwa wapo njiani kuelekaia Wilaya ya misungwi.
“Gari imeharibika safarini kuelekea misasi wilaya ya misugwi”
Jionee baadhi ya picha za hivi karibuni za wakali hawa hapo juu.
Unadhani ni kweli kazi ya jamaa hawa itakuwa kali ya mwaka!!!
No comments:
Post a Comment