Polisi wa kimataifa , interpol tawi la Tanzania wamemkamata mfanya biashara maarufu raia wa Kenya kwa tuhuma za kujihusisha na ujangili na uhalifu uliovuka mipaka ,hususan mauaji ya tembo .
mtuhumiwa huyo Mohamed Ally Feisal Amekamatwa mjini Dar-Es-Salaam baada ya kusakwa kwa kipindi kirefu kwa makosa hayo ya kimataifa kutoka Dar Regina Mziwanda anaarifu zaidi.
Akitbibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo Bwana Diwani Athumani kutoka kamisheni ya Kurugenzi ya makos aya jinai amesema mtuhumiwa huyo anakabiliwa na tuhuma za kujihusisha na vitendo vya uhalifu wa kimataifa ikiwemo uwindaji wa uliovuka mipaka kimataifa katika nchi mbali mbali)
Bwana Athumani Diwani alieleza kuwa kwa sasa mtuhumiwa huyo anashikiliwa huku upelelezi ukiendelea kujua makosa mengine aliyoyafanya kuhusiana na biashara za bidhaa zitokanazo na Tembo ndani ya Tanzania na katika nchi nyingine za Afrika Mashariki ikiwemo nchi yake ya asili Kenya.
Mohamed Feisal Ally amekuwa akitafutwa kwa muda mrefu kwa tuhuma za uwindaji haramu husani mauaji ya Tembo tatizo ambalo ni kubwa hususani katika ukanda huu wa Afrika Mashariki hasa Kenya na Tanzania ambapo idadi kubwa ya Tembo wamekuwa wakiuawa kila mwaka na kutishia kutoweka kwa viumbe hao.
No comments:
Post a Comment