TTCL

EQUITY

Sunday, November 23, 2014

Mtoto aliyekufa kwa ajali azikwa Uganda

wanawake wakiandamana huku wakiomboleza nchini Uganda
Shughuli za mazishi ya mtoto wa miaka miwili zimefanyika nchini Uganda, mtoto ambaye kifo chake kimezua ghadhabu baada ya mtoto huyo kugongwa na gari la halmashauri ya jiji la Kampala ,baada ya mama yake kukamatwa akiuza matunda kinyume cha sheria.
Familia ya Ryan Ssemaganda na wanasiasa wa upinzani walitishia kutomzika mtoto huyo mpaka maofisa hao watakapo wajibika kwa kitendo hicho.Mwili wake ulichukuliwa wakati wakiandamana kuelekea bungeni siku ya alhamisi.
Raia wa Uganda wanaona kuwa halmashauri hiyo inatumia nguvu nyingi kupambana na wachuuzi wa mitaani.
Mama wa mtoto Ryan alikamatwa siku ya jumatatu baada ya kukutwa akiuza matunda huku akiwa hana leseni.
Siku iliyofuata, Bibi wa mtoto huyo alimpeleka katika Ofisi za Mamlaka ya mji wa Kampala ambako mama mtoto alikuwa akishiliwa , nia ilikua kumpa mama mtoto ili amnyonyeshe.
Maafisa wa Ofisi hiyo walikataa na wakati wakijadiliana kuhusu hilo, mtoto alichoropoka kutoka kwa mama yake na kugongwa na gari linalomilikiwa na Mamlaka hiyo.
Siku ya Alhamisi polisi ilizuia kupelekwa kwa mwili katika Bunge, wakisisitiza mwili huo uzikwe ili marehemu apumzike kwa amani, na kuwataka waepuka jambo hilo kushughulikiwa kisiasa.

No comments:

Post a Comment