Watu wawili wanashikiliwa na Polisi nchini China baada ya kuwafungulia mamia ya Panya katika kijiji kimoja.
Wakazi wamesema zaidi ya Panya 1,000 walifunguliwa katika kijiji kimoja kusini mwa jimbo la Guangdong, tovuta ya gazeti la Guangzhou limeripoti.
Mwanakijiji mmoja amesema zaidi ya Panya 1,000 walikuwa wakikimbia huku na huko, hali ilikua mbaya.
Mamlaka ya afya imepeleka sumu katika eneo hilo ili kupambana na Panya hao ikihofu kuwa wanaweza kusambaza maradhi.
Watu wengine watatu wanaohusishwa na tukio hilo wamekimbia kijiji hicho,na sababu ya kuwafungulia panya hao hazijajulikana.
Lakini ripoti zinasema Watu wanaoshikiliwa wameiambia Polisi kuwa waliwafungulia Panya kikiwa ni kitendo kutoa sadaka ili ndugu yao apate ahueni.
Kuwatoa wanyama kwenye mazingira waishio binadamu kinahesabiwa kuwa kitendo cha kujitolea na matukio haya ni maarufu hata hivyo yamekua yakiharibu mazingira.
No comments:
Post a Comment