Mabaki ya ndege ya MH 17
Shirika la ulinzi la ulaya,limearifu kwamba mabaki ya ndege ya shirika la ndege la Malaysia yaliyookotwa huko mashariki mwa Ukraine hatimaye yanarejeshwa Uholanzi.
Mkuu wa shirika hilo Michael Bociurkiw ameiambia BBC mabaki yaliyokusanywa na timu ya uchunguzi kutoka Ujerumani, ambao wamekwisha ingia katika ardhi inayo dhibitiwa na serikali ya Ukraine na mabaki hayo yatasafirishwa kwa ndege kutoka katika mji wa Kharkiv.
Timu hiyo ya watafiti wa Kijerumani inaongoza timu ya watafiti wa kimataifa kufuatia ajali hiyo ya ndege iliyotokea mwezi July kutokana na maombi maalumu ya serikali ya Ukraine.
Ndege hiyo iliondoka katika uwanja wa Amsterdam na idadi kubwa kati ya abiria 298 ya waathirika wa tukio hilo ni Wajerumani .
Juhudi za uchunguzi huo zinakwamishwa na mgogoro unaoendelea huko Mashariki mwa Ukraine kati ya Urusi na nchi hiyo mgogoro ambao unaungwa mkono na askari wa majeshi ya nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment