TTCL

EQUITY

Sunday, November 2, 2014

Kweli mfa maji hutapatapa atimaye ccm waanza kulazimisha maoni yao


Tokea nizaliwe sijawai kukasirishwa na hili jambo la Makonda kumpiga na chupa Mzee Warioba. Ni utovu wa nidhamu, ni dharau, ni ujinga, ni utoto, ni ukora, ni u.p.mbavu, ni akili ndogo, ni kukosa hekima na misamiati ya namna hiyo kwa hili jambo la Makonda kumpiga na chupa mzee Warioba. Nilikuwepo kwenye eneo la tukio kwa macho yangu nikashuhudia Makonda akimpiga na chupa mzee Warioba, nimeumia sana sana. CCM lazima waruhusu mawazo mbadala ili kujenga Taifa na kamwe kundi moja lenye mawazo yanayofanana hauwezi kujenga Taifa, lazima kuwepo na mawazo huru kwa pande zote katika jamii. 

Ila nasita kusema kama kweli Makonda katumwa na CCM inawezekana kabisa katumwa na Nape au Sita. Warioba ni Kiongozi mstaafu tena katumikia Tanzania kwa moyo wote hivyo vijana kukosa adamu mpaka kufikia hatua ya kumpiga na chupa ni ujinga wa hali ya juu na vijana wa pande zote lazima tukemee hili jambo. Jeshi la polisi tafadhali mlifanyie hili kazi, na Makonda naomba nikupe ujumbe kuwa vijana hatutakaa kimya lazima tutakufanya kwa njia yoyote ile uweze kumuomba Mzee Warioba radhi na taifa kwa ujumla, Leo umefanya kwa Warioba, Kesho utasita kufanya kwa Mwinyi au Malecela au Mkapa...


Nimeuzunishwa sana na hili jambo....Shame on you Makonda

Maneno ya Butiku naomba kunukuu "Huu uhuni uliyofanywa na Makonda haukubaliki hata kidogo, kitendo cha kumpiga Warioba na chupa tunaomba serikali iliangalie jambo hili na pia kuhakikisha katika midahalo mingine huyu muhuni asiwepo, Asanteni" mwisho wa kunukuu. 

Maneno ya Butiku baada ya kikao kuisha akiongea na vijana nje ya ubungo plaza

Naomba kunukuu "Kamwe vijana wa CCM msikubali kuchagua viongozi wanaomtuma Makonda kutenda haya, ni uhuni na ujinga wa hali ya juu" alipoulizwa ni nani wako nyuma ya Makonda, bila kusita akasema Membe na Sita



Baada ya tukio hilo vijana wengine ambao wanaona haifai wakawavamia hao wenye mabango kua katiba inafaa....
Wakati mvutano huo unaendelea yule mbunge wa bunge la katiba mwenye ulemavu wa macho nae kavamiwa akaanza kupigwa .......


Wakati haya yote yakiendelea Makonda poul alikua yupo pembeni, baada ya kuona vijana wakimpiga mlemavu akaamua kuingilia kumuokoa mlemavu wakati hayo yote yakiendelea warioba alikua ametoka ukumbini hivyo si sahihi kusema makonda kampiga na chupa warioba.. maana warioba na butiku walitolewa mapema vuguvugu lilipoanza... ocampo ufor wacha uongo ....

Kitendo cha makonda kutaka kumwokoa mlemavu vijana wakamvamia kuanza kumpiga pia makonda.....

Kwa hali ilivyo wanzalishi wa vurugu ni vijana waliwavamia walioweka mabango kusema katiba inafaa.... je wasingewavamia kuna athari gani kwa nini waliwazuia wakati ni haki yao ya msingi kuwakilisha mawazo yao kikatiba...

Je ni busara kumpiga mlemavu kwa kua alishiriki bunge la katiba.... vijana wanampiga mtu asie ona. Je makonda kuamlia ugonvi mlemavu asipigwe kosa lake lipi?

Taifa linaharibika vyama vinatugawa ukisema katiba nzuri wewe ccm ukisema mbaya we ukawa sio sahihi..... 

Bado nipo ubungo unaweza niuliza lolote,,,,

Nimesikitika kumwona okampo ufoo akipotosha umma....kwa siasa za chuki

No comments:

Post a Comment