TTCL

EQUITY

Sunday, October 19, 2014

FIESTA YAFANA DSM,DAVIDO,ALI KIBA,DIAMOND WAZUA GUMZO KWA MASHABIKI,T.I AWAKUNA WABONGO


Msanii wa muziki kizazi kipya,Rachael kutoka THT akitumbuiza jukwaani kwenye usiku wa tamasha la Fiesta 2014 lililofanyika katika viwanja lidaz Club,Kinondoni jijini Dar.


Mmoja wa wasanii wa kike wanaofanya vyema katika anga ya muziki wa Bongogfleva,Shah akiwa na skwadi lake wakilishambulia jukwaa la fiesta usiku wa kuamkia leo. 


Mkali mwingine wa steji,ambae amekuwa akifanya vyema kwenye matamasha mbalimbali ya fiesta,ukipenda muite Kabyser ama Mr Blue akiimba jukwaani mbele ya umati wa watu waliofika kwenye tamasha la Fiesta 2014,ndani ya viwanja vya lidaz club jijini Dar 


Mkali mwingine wa hip hop nchini Mwana-FA akiwaimbisha mashabiki wake (hawapo pichani) usiku wa kuamkia leo kwenye tamasha la Fiesta 2014 


Kama kawaida yao wawapo jukwaani,ni kushambulia jukwaa mwanzo mwisho,pichani kulia ni Stamina na Ney wa Mitego wakikamua jukwaani. 


Abdulkiba nae akionesha yake jukwaani 


Ilikuwa ni shoo moja nzuri kutoka nyumba ya vipaji ya THT 


Ilikuwa buruuudani kabisa 


Pichani msanii Linah (nyeupe) akiwa na skwadi lake mara baada kumaliza kulishambulia jukwaa kwa pamoja. 


Anaitwa Ally kiba ambaye inaelezwa kutoka kwa mashabiki kuwa alifanyo shoo nzuri na iliyowavutia,na kuthibitisha uwezo wake kuwa ni kweli amerejea kwenye kiti chake cha usanii. 


Mashabiki wakifuatilia tamasha la Fiesta 2014. 


Majina yote mpe yeye,mara Dangote,mara Chibu afu jazia na diamond Platnum akiwa kazini na skwadi lake zima la kazi, Palikuwa hapatoshi na hayo magamba.


Msanii kutoka nchini Marekani Clifford Haris a.k.a T.I akiwasili kwenye viwanja vya lidaz club Kinondoni jijini Dar kutumbuiza tamasha la Fiesta lililofanyika jana. 


Msanii kutoka nchini Nigeria, David Adedeji Adeleke a.k.a Davido akiwakuna mashabiki wake kwa kucheza staili yake ya Skelewi jukwaani,huku miluzi na shangwe ikiwa imetawala kila kona ya uwanja. 


Davido na Diamond wakilishambulia jukwaa kwa paoja. 





Msanii kutoka nchini Marekani Clifford Haris a.k.a T.I akilishambulia jukwaa la Fiesta vilivyo 


NO MEDIOCRE




Mashabiki nao walishangweka kwa raha zao 


T.I akiwaimbisha mashabiki wake (hawapo pichani ) na wimbo wake wa NO MEDIOCRE. 



Pichani juu na chini ni sehemu ya umati wa watu wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye tamasha fiesta usiku wa kuamkia leo,lililofanyika katika viwanja vya Lidaz Kinondoni jijini Dar. 



Ilikuwa ni sheeeddddaaa.


Shaha na skwadi lake wakilishambulia jukwaa 


Ommy Dimpoz na Victoria Kimani wakilishambulia jukwaa la fiesta 2014 


Palikuwa hapatoshi 


Victoria Kimani akilishambulia jukwaa 


Palikuwa hapatoshi jukwaani kwa kila aina ya burudani 


Mmoja wa askari waliokuwa wamepangwa katika suala zima la kusimamia usalama ndani ya tamasha la Fiesta 2014 akihakikisha usalama wa kutosha unakuwepo katika eneo hilo,na watazamaji wanapata burudani iliyokusudiwa kutoka kwa wasanii mbalimbali waliotumbuiza usiku wa kuamkia leo. 


Shaa na madansa wake wakilishambulia jukwaa 


Msanii kutoka THT,Barnaba akiimba wimbo wake wa Wahalade sambamba na madansa wake kwenye jukwaa la fiesta 2014,katika viwanja vya Lidaz Kinondoni jijini Dar.
19 Oct 2014

No comments:

Post a Comment