TTCL

EQUITY

Wednesday, November 5, 2014

Filamu ya ‘Girlfriend Part 2’ ya TID kuingia sokoni hivi karibuni



TID yupo mbioni kuachia filamu ya ‘Girlfriend Part 2’. Filamu hiyo itakuwa muendelezo wa filamu inayotajwa kuwa ya kwanza kuwashirikisha wasanii na miongoni mwa filamu za awali kabisa za Tanzania.

Pamoja na TID aliyekuwa muigizaji mkuu na aliyeigiza kama msanii anayetafuta njia za kutoka, filamu hiyo iliwashirikisha mastaa kama AY, Crazy GK, Monalisa na wengine.

Katika Girlfriend Part 2, TID ataigiza na msanii wa Bongo Movie, Sabby Angel aliyeigiza filamu kama Siri ya Giningi, Moto wa Radi, Sio Riziki. TID amesema filamu hiyo itaingia sokoni hivi karibuni.

Katika hatua nyingine, msanii huyo anatarajia kuachia video ya wimbo aliomshirikisha msanii wa Kenya, Nazizi. Miaka kadhaa iliyopita muimbaji huyo ambaye jina lake halisi ni Khalid Mohamed alimshirikisha msanii huyo wa Kenya kwenye wimbo wake ‘Watasema Sana’ uliofanya vizuri kwenye nchi za Afrika Mashariki.

Wawili hao wamekutana tena kufanya wimbo mpya uitwao ‘Pressure’. Video ya wimbo huo imeshafanyika na itazinduliwa November 30. Pressure ni wimbo utakaopatika kwenye album yake mpya ‘Mnyama. 

No comments:

Post a Comment